KATA YA KISIWANI KUENDELEA KUNEEMEKA

KATA YA KISIWANI KUENDELEA KUNEEMEKA

🔶Kikundi cha wanawake cha KUHAWA kilichopo Kata ya kisiwani kitaendelea kupokea ufadhili wa wadau wa maendeleo kutoka Uholanzi katika nyanja za Ujasiliamali, Afya, Elimu na huduma nyingine.

🔶Dhamira hiyo imesemwa na Mama Tushi na baba Harry - raia wa Uholanzi walipokuja kutembelea kikundi hicho.
Hadi sasa wadau hao wamesha jenga wodi la wanawake Kisiwani, madarasa 2, kituo cha kupimia afya, kompyuta 21, huduma kwa watoto wa mazingira magumu na WAVIU.
Kwa sasa wameahidi kujenga jengo la kujifungulia na kuendelea kuleta kompyuta kwa ajili ya shule.

🔶DC wa Same aliyekuwa mgeni wa shughuli hiyo alisisitiza umuhimu wa kufuata taratibu za nchi kila wanapokuja; viongozi wa kijiji na kata kuwapa ushirikiano na aliwashukuru kushirikiana na serikali katika kufikisha huduma kwa wananchi.

🔶Aliwataka kupanua wigo wa huduma zao. Na kuunga mkono juhudi za Tanzania ya viwanda zinazoongozwa  na Mh Dr. John Pombe Magufuli kwa kuwanunulia wanawake wa KUHAWA mashine ili waanzishe kiwanda.
Hili pia litaleta uendelevu wa huduma wanazozitoa.

Kikundi cha KUHAWA kimeaswa kutoa taarifa serikalini kwa kila wanachokifanya.

WANAWAKE WANAWEZA

Maoni