Kitambilisho cha Taifa hakihalalishi uraia


                                    Kamanda wa Uhamiaji Kiteto, Ikomba Mathew ..


Na, MOHAMED HAMAD
Sheria za Tanzania, makundi matatu ndio yanastahili kupata kitambulisho cha Taifa kinachoweza kumtambulisha  mtu uwepo wake hapa nchini.
Makundi hayo ni Mtanzania mwenyewe, mtu aliyekimbia nchi yake (mkimbizi) na raia wa kigeni wanaoishi nchini kwa mujibu wa Sheria (walowezi), kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza na MTANZANIA, Ikomba Mathew Kamanda wa Uhamiaji Kiteto alisema, Mkimbizi sio Raia wa Tanzania, sambamba na waliopewa  vitambulisho vya Taifa.
“Utaratibu unataka baada ya zoezi la uandikishaji vitambulisho vya Taifa, fomu zitarudishwa kwenye kamati za ulinzi na usalama za kata ili zichambuliwa kubaina raia na wasio raia wa Tanzania”.
 Alisema walowezi watakao jiandikisha hawatopata vitambulisho mpaka wawe na vibali vya ukaazi, hivyo watakapojificha kama wahamiaji walowezi kitambulisho cha Taifa hawatopewa.
Majina yatabandikwa kwenye mbao za matangazo ili watu waweze kuhakiki, akisema nchi hii haihitaji raia wengine kama alivyosisitiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli kuwa akinamama zaeni.
“Ndio maana vituo vya afya vinajenga na hata kuboreshwa, ili Serikali iweze kutoa huduma kwa kiwango stahili..kwahiyo, naomba majina yatakaporudi kwa haki kabisa sema huyu sio raia wa Tanzania vyombo vya Ulinzi na Usalama vipo?.
Kwa upande wa baadhi ya wananchi walisema, Wilaya ya Kiteto ni korido la kupitisha wakimbizi, ambapo walishughudia kila mara kumatwa na kufunguliwa mashtaka.
Salimu Mbwegu Mwenyekiti wa Kijiji cha Dosidosi, alikiri wakimbizi kupitishwa katika eneo lake na alipoweza kuwabaini alitoa taarifa..huku Hamza mngia (mwananchi) akisema hiyo ni biashara
“Tunasikia watu wanaopitishwa humu, huwa ni biashara, hapa tulishughudia zaidi ya miili 40 ya waliokufa baada ya kukosa hewa wakiwa kwenye magari walipokuwa wanasafirishwa kwenda Afrika ya kusini”
Mwisho.

Maoni