(MB) Mahawe atoa msaada wa mashuka ya wagonjwa Mirerani

Na Mohamed Hamad

MUNGE wa viti maalumu Ester Mahawe (CCM), amekabidhi Msaada wa shuka 20 Waziri Jenista Mhagama kwaajili ya word ya wanawake kujifungua kituo cha Afya Mirerani.

Shuka hizo zilikabidhi Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Sera na Uratibu wa Binge Mhe Jenista Mhagama alipofika kuweka jiwe na msingi katika kituo hicho.

Akizungumza mbele ya Waziri Mhagama, mbunge Ester Mahawe, aliipongeza Serikali ya awamu ya tano kwa jitihada za ujenzi wa kituo hicho.

Alisema kituo hicho hakikuwa na gari la wagongwa hali iliyowapa wananchi usumbufu mkubwa hivyo baada ya kuomba gari la wagonjwa bungeni lilitolewa na Rais hivi karibuni.

Alisema usikivu wa Serikali ya awamu ya tano ya Dr John Pombe Magufuli umempa matumaini makubwa hali iliyomfanya aunge mkono kuwapa shuka hizo kwaajili ya wanawake.

Serikali mbali ya gharama iliyotumika katika ujenzi huo kupitia TACAID walitoa zaidi ya mil 200 ambapo pia walitoa shuka 100 huku ofisi ya mkuu wa Mkoa ikitoa shuka 50 na umoja wa vijana 20.

Akizungumza na wananchi wa Mirerani, Waziri Mhagama alisema kukamilika kwa kituo hicho kutasaidia wananchi elfu 49 ambao awali walikosa huduma hiyo.

Alielezwa kuwa wananchi wa Mirerani wanakabiliwa na tatizo la ugonjwa wa kifua kikuu kutokana na kazi wanazozifanya ambazo ni uchimbaji wa madini.

Pia tatizo lingine na hatari zaidi ni ugonjwa wa upungufu wa kinga mwilini Ukimwi unaotokana na mwingiliano wa watu katika shughuli ya madini.

Katika hatua hiyo Waziri Mhagama ametoa wito kwa wananchi hao kupima afya zao sambamba na kulinda afya kwa kuacha ngono uzembe

"Wanaume mmekuwa na tabia ya kutopima afya na kutuma wake zenu kupima ili mjue kama mko salama, huu sio utaratibu mzuri pimeni wote"

Alisema Serikali imejipanga kuanzisha mpango maalumu wa wanaume kupima afya zao baada ya jitihada kubwa za upimaji kufanyika kwa wanawake.

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa TACAID alimweleza Waziri Mhagama kuwa ujenzi wa kituo hicho umetokana na uhitaji mkubwa wa wananchi baada ya kufika na kuomba hitaji la huduma hiyo.

Mhe Waziri baada ya kufika hapa tulikuta hali mbaya sana ya huduma duni ya afya hivyo TACAID kwa kuona haya ndipo tukanzisha ujenzi huo, alisema Mkurugenzi

Kwa upande wa wananchi hao walipongeza Serikali kwa kujenga kituo hicho wakisema awali walipata shida kubwa kupata huduma hiyo kwa gharama kubwa kufuata Huduma maeneo mengine

Kituo hicho kimewekwa jiwe la msingi na Waziri Mhagama akisema lengo la Serikali ni kuharakisha kukamilika ili huduma hiyo ianze kutolewa kwa watu wanaokadiriwa 49,000.

Mwisho.

Maoni