MRADI WA MAJI HEDARU KUKAMILIKA 30/05/2018




MRADI WA MAJI HEDARU KUKAMILIKA 30/05/2018Ziara ya kukagua mradi wa maji  Kijiji cha Hedaru unaogharimu Tshs. 1.18 B. Ni mradi wa vijiji 10 ambao ulitakiwa kuisha tangu 2015.

DC Same Mh. Rosemary Senyamule Akikagua mradi huo ataka mkandarasi kuhakikisha maji yanatoka sasa na yataendelea kutoka wakati wa kiangazi. 

Kwani Wananchi wahofia kama kweli mradi utatoa maji wakati wa kiangazi.
Kamati iliyoundwa kusimamia maji  yaagizwa kukagua maeneo yote na kutoa taarifa kwa Eng. kabla mkandarasi hajakabidhi ili akabidhi mradi usio na kasoro.

DC akagua agundua mifumiko mingi imevunjika, koki nyingi zimeibiwa, apokea taarifa ya maeneo/ vituo visivyotoa maji. 

Mji wa Hedaru ni mji unaaongoza kwa kukua kwa kasi Wilayani Same.
Eng. Mussa aeleza jinsi mradi huo utakavyoongezewa nguvu na tanki lingine linalojengwa mwaka huu, ili kukidhi ongezeko la watu.

"Mradi huu ni kati ya miradi iliyokuwa imeainishwa kwenye ilani ya CCM 2010- 2015. Hivyo atakayecheza nao tutamshughulikia." Alisema DC Huyo.

Maoni