Askofu Mkuu Wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) nchini Dr.Barnabas Mtokambali, ameweka Jiwe la msingi shule ya Sekondari ya Great Nation Seminary Wilayani Simanjiro.
Shule iko kijiji cha LOBOSOIT A kata ya Emboreet, ambayo inatarajiwa kuanza rasmi Januari 2019 kwa mchepuo Wa sayansi na kilimo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Bw. Myenzi kwa niaba ya Serikali alisisitiza kuwa viongozi wa shule hiyo wazingatie viwango bora vya elimu.
Alisisitiza maadili na uzalendo kwa wanafunzi akisema watakaodahiliwa shuleni hapo wawe na tija na ufanisi wa kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla
Alisisitiza kuwa pawepo na gharama nafuu ili wananchi wa Wilaya ya Simanjiro wamudu kupeleka watoto wao shule na kudiwe na kikwazo kufanya watu wasinufaike na shule hiyo.
"Napenda kuona mitaala inayoendana na azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuzalisha wasomi watakaolisaidia taifa kujenga uchumi wa viwanda".
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Myenzi sekondari hiyo ni ya 18 kwa Wilaya ya simanjiro, ambapo alidai jitihada za kuongeza zingine zinaendelea.
Ujenzi wa shule Hiyo unatajiwa kugharimu kiasi cha sh 2 bilioni hadi utakapokamilka na kwamba kwa sasa unafanywa kwa awamu.
Kwa sasa majengo ya madarasa 3, jengo la Utawala, bweni la wasichana na vyoo vya wanafunzi yamekamilika huku maabara tatu zikiwa kwenye hatua za umaliziaji.
Kiongozi huyo wa kiroho, Baba askofu aliahidi kuchangia milion 50 Kuendeleza ujenzi kwa shule hii ya jimbo la TAG kaskazini kati.
WILAYA YA SIMANJIRO INA SHULE ZA SEKONDARI 17 KATI YAKE 15 ZA SERIKALI NA 2 ZA BINAFSI HIVYO SHULE HII ITAONGEZA IDADI IDADI YA SHULE NA KUPANUA WIGO WA ELIMU KWENYE ENEO HILI LA JAMII YA WAFUGAJI.
Maoni
Chapisha Maoni