CRDB KITETO WAFUTURISHA..

Benki ya (CRDB) Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imeandaa futari na kufuturu pamoja na baadhi ya wananchi wa mji wa Kibaya.

Meneja wa CRDB Kiteto, Bi Lucy akizungumza na wananchi hao baada ya futari alisema, wameamua kufuturu pamoja kama njia ya kujema mahusiano ya karibu na wananchi.

"CRDB tunafanya kazi na jamii hivyo tumependa kuwahakikishia kuwa tupo pamoja na tutaendelea kuwa pamoja katika huduma ya Kibenki.

..CRDB tuna fursa nyingi kama vile, mikopo, akaunti ambayo haina  makato pamoja na huduma  zingine muhimu"

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Tumaini Magesa alikuwa mgeni rasmi, pamoja na mambo mengine alipongeza taasisi hiyo  ya CRDB na kuomba zingine kuiga.

Shekh Juma Mohamed Hicha ni Shekh wa Wilaya ya Kiteto akizungumzia futari hiyo alisema inafaa kuigwa kwani fadhila ni nyingi kwa Mungu.

Mkurugenzi mtendaji wa halm ya Wilaya ya Kiteto tamimu Mahmoud Kambona alisema kama wadau wa maendeleo wataendelea kuwa karibu na wananchi katika kuwahudumia.

Mwisho.

Maoni