DC Mbulu ashusha bei ya nyama.
Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara Be. Chelestino Mofuga ameagiza wafanya biashara ya nyama kuuza kilo moja sh 6000 kutoka 7000.
Hatua hiyo imetokana na kukutana na wafanyabiashara hao wa nyama na kujadili changamoto wanachokabiliana wafanyabiashara hao
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa community center katika Halmashauri ya mji wa Mbulu Juni 6 mwaka huu.
Mkuu wa wilaya mwanzo aliwataka wafanyabiashara hao kutoa sababu za msingi zinazowafanya bei ya nyama Mbulu iwe juu kuliko sehemu nyingine bila majibu ya msingi.
Kutokana na amri hiyo wafanyabiashara hao akiwemo Philipo Shauri alisema bei ya nyama iko juu kwa sababu Ng'ombe kwa wilaya ya Mbulu hawapatikani kama ilivyodhaniwa na wengi.
Wakati wa mvutano huo wafanyabiashara hao hawakuonyesha utayari wa kupunguza bei hiyo kutoka 7000/ baada ya Mkuu wa wilaya kuonyesha msimamo wake bei ilipendekezwa kuwa iwe 6000/ kwa kg moja.
Wafanyabiashara hao waliomba wiki moja kabla ya kushusha bei ili wajiandae kwa mabadiliko mpya ya bei na Mkuu wa Wilaya akawapa siku saba kutoka tarehe 6.6.2018 hadi 13.06.2018.
Mkuu huyo wa Wilaya Bw. Mofuga alihitimisha kwa kuwataka wafanyabiashara hao kutii makubaliano hayo yaliyoafikiwa na pande zote mbili.
Maoni
Chapisha Maoni