DC Kiteto atoa hofu wananchi wa Ilkiushbour

Mkuu wa Wilaya ya Kiteto, Eng Tumain Magesa amewatoa hofu wananchi  wa Kijiji cha Ilkiushbour wanaoishi mpakani mwa hifadhi ya wanyama Mkungunero kuwa Serikali inawalinda hadi watakapofidiwa kuondoka katika maeneo hayo.

Msichunge kwenye hifadhi ya Mkungunero ni kosa kisheria, na wala msitumie nguvu kushuhulika na hili jambo, liachieni Serikali ya Kiteto nitawalinda.

Hatua hiyo imefikiwa na mkuu hiyo wa Wilaya Kufuatia malalamiko ya wananchi hao kuwa wananyanyaswa na baadhi ya askari wa Hifadhi.

"Mhe DC..hapa tulipo hatuna amani, tunapigwa, kuporwa mali zetu kila mara na askari hawa..mateso tunayopata utadhani hatupo ndani ya nchi yetu.

"Wazee wananyanyasika, wanadhalilishwa wanapokutana wanaamriwa kuchapana na watoto wao wadogo na askari hao jambo ambalo limekuwa tishio"

Walisema matamko ya viongozi wa Taifa yanawachanganya, kwani awali Waziri Mkuu alitoa maelekezo kuwa wananchi waliopo mpakani mwa hifadhi wasibughudhiwe.

Waziri wa Maliasili Hamis Kigwangala naye alipofika maeneo hayo aliwataka wananchi hao kuondoka huku mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti akiwatoa hofu kuwa wasiondoke.

"Mimi ndio Mkuu wa Mkoa wa Manyara, wananchi tulieni..mtaondoka kwa utaratibu maalumu wa Kiserikali, acheni taratibu za Kiserikali zifanyike" alisema RC Mnyeti.

Kwa kipindi chote wananchi hao wamedai wamekuwa wakinyanyasika dhidi ya askari hao kuwakamata wakiwa hata nje hifadhi hiyo.

Hali hii imemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kufika na kuwatoa hofu akiagiza uongozi wa hifadhi hiyo kuacha kuwakamata wananchi katika maeneo yao hadi taratibu za kisheria zitakapofanyika.

Tuliambiwa tuje kuwapa elimu na taatifa sahihi hawa wanachi maamuzi ya Serikali sambamba na kuanza kurejesha alama..dio kuwakamata. Naomba wasikamatwe tens.

"Wananchi waachwe, wasibughudhiwe katika maeneo yao...naomba viongozi wa Mkungunero naona kuna wawakilishi hapa acheni kukamata wananchi hawa mpaka mfanye mlichoagizwa"

Awali eneo hill lilionekana kung'olewa alama zake hivyo kutakiwa kurejeshwa ili ijulikane kuwa waliopo katika maeneo hayo nani yuko ndani aondololewe.

Alama zitakapobainishwa hatua itakayofuata ni makubaliano ya fidia kwani ninyi wananchi mmekutwa na hifadhi hii ya Mkungunero, alisema DC Magesa

Kwa upande wake Donosani Makori Afisa wanyama Pori wa Mkungunero alisema malalamiko hayo hayana ukweli ingawa suala hill liko mahakamani kuhusu madai ya kuporwa mifugo yao.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Ilkiushbour akizungumza kwenye mkutano kati ya uongozi wa Kiteto pamoja na Uongozi wa hifadhi hiyo alisema amechoshwa na manyanyaso wanayopata wananchi toka kwa askari hao

"Hivi kama Kijiji ndicho chenye sheria ya kulinda mipaka yake, Mkungunero wanapata nguvu wapi kuja kuweka alama kijijini bila hata kutushirikisha viongozi " alihoji

Mwisho.

Maoni