KUFANYA KAZI KWA FAIDA NA MAENDELEO YETU SI UTUMWA

KUFANYA KAZI KWA FAIDA NA MAENDELEO YETU SI UTUMWA

👉🏼Ni maneno yaliyosemwa na wananchi wa Kijiji cha Mhezi walioamua kukusanya mawe kwa ajili ya ujenzi wa shimo la kutupa kondo la nyuma na jengo la kuchomea taka katika zahanati ya Mhezi, kila nwananchi alipangiwa kukusanya mawe 30 kama mchango wake.

👉🏼DC wa Same Mh. Rosemary Senyamule aliyeamua kushirikiana na wananchi wa Wilaya yake kila jumatatu kwa kufanya kazi za kijamii, alishiriki kazi hiyo ya kusomba mawe kwa kiwango sawa na wananchi wengine.

👉🏼" Kama tulitumia nguvu zetu nyingi kufanya kazi kwa faida ya wengine utumwani; hebu sasa tutumie nguvu ile ile kufanya kazi kwa maendeleo yetu. Hakika tutaona maendeleo ya haraka Same" Alisema DC huyo.

👉🏼Aliwaasa viongozi wa vijiji na kata kushirikiana na wananchi kwa kufanya nao kazi na sio kuwasimamia. Kwa kusema, uongozi ni vitendo na sio maneno.

👉🏼Baada ya kazi hiyo DC pamoja na wataalamu alioongozana walitumia nafasi hiyo kusikiliza kero za wananchi wa Mhezi na kuzitolea majibu

👉🏼Wananchi wa Mhezi waliipongeza serikali ya awamu ya tano na Mh. Rais John Magufuli kwa kupata huduma ya maji maeneo mengi pamoja na mradi tarajiwa, pia waliomba kupata umeme maeneo yaliyobaki.

" Same is not the same"

Maoni