OLENGAPA YALETA WATU KUTOKA NJE KUJIFUNZA..

OLENGAPA NI NINI?

✍🏿Olengapa ni nyanda za malisho ya pamoja zilizoundwa na vijiji 4 wilayani Kiteto Mkoani Manyara.

✍🏿Vijiji hivyo ni Lerug, Orkitikiti, Ngapapa na Engongangare

✍🏿Lengo la la vijiji hivyo ni kuwa na nyanda ya malisho ya pamoja kupunguza migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji

✍🏿Kimsingi eneo hili liliundwa mwaka 2013 chini ya shirika la Kinnapa kwa kushirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo

✍🏿Eneo la Olengapa litatumika kwaajili ya  mifugo na kwa mipango ijayo kutakuwa na majosho, pamoja na kupandwa majani kwaajili ya mifugo.

✍🏿Akizungumza na viongozi wa Serikali pamoja na wakuu wa mshirika yasiyo ya Kiserikali ya ndani na nje ya nchi, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mhandisi, Tumaini Magesa, alisema anatamani kuona Kiteto inapata maendeleo ndani ya utaratibu

✍🏿"Naogopa sana kwenda nje ya utaratibu halafu tukapata maendeleo, ni sawa na MTU anachumbia binti yako akatoa mahari kisha akamuua"

✍🏿Kwa hiyo lazima tufike mahali tufanye vitu vyetu sawia na ndani ya eneo letu bila kutokea madhara yoyote"

✍🏿Hatua hiyo imetokana na hatua mbalimbali zilizofikiwa na uongozi wa Olengapa, Serikali pamoja na wadau wa maendeleo katika kuunda nyanda hiyo ya malisho Olengapa

✍🏿Jumla ya watu 22 wa ndani na nje ya Nchi wakiwemo viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali, wamewasili wilayani Kiteto kujifunza namna nyanda hiyo ya malisho ilivyoundwa

✍🏿Kwa kawaida Mara nyingi kwa kawaida kuunda eneo moja lenye malengo yanayofanana vijiji zaidi ya kimoja huwa vigumu ila limewezekana Kiteto na sasa watu wanatoka nje ya nchi kujifunza

Watu hao wametoka nchi mbalimbali za Bara la Afrika ambao ni wakuu wa mashirika

✍🏿Kimsingi eneo hili lina ukubwa wa hekta 30 sawa na ekari elfu 75 ambalo sasa wamepanda nyazi za malisho ekari 1.5 kama mfano

Kwa sasa maeneo mengine mawili yamebainishwa kutaka kuanzishwa baada ya kuona mpango huo kuwa utakuwa na tija...

FUATANA NAMI KATIKA MPANGO HUU..🤝🏿🤝🏿🤝🏿

Maoni