Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mh Chelestino Mofuga leo tar 01/6/2018 amefanya kikao cha kazi na watendaji wa serikali wilayani humo
Miongoni mwa walioshiriki ni madiwani wote, Wakurugenzj, wakuu wa idara wote , watendaji wa vijiji na kata , wakuu wa shule na wenyeviti wote.
Lengo la kikao hicho ni kukumbusha wajukumu ya kuwatumikia wananchi kwa kuwaletea maendeleo.
Akiongea katika kikao hicho Mkuu huyo wa Wilaya amewataka watumishi wote na viongozi kushuka kwa wananchi kusikiliza kero na kuzitatua.
Pia amewataka wakuu wa shule kuhakikisha wanawasimamia vizur walimu ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa asilimia 80.
Mkuu huyo akijibu hoja ya malalamiko kuhusu jeshi la polisi dhidi ya bodaboda, kuwa wananchi na viongozi wa ngazi zote wanapaswi kusaidia kuwaelimisha vijana wa bodaboda kufuata sheria badala ya kuwaona polisi ndio wakosaji wanapotimiza wajibu wao wa kuzuia ajali.
Amesema wapo polisi ambao wanakiuka sheria ya kazi lakini wachache hivyo sio vema kulaumu jeshi lote la polisi.
Amewataka wananchi kutambua polisi ni watu sawa na watumishi wengine, wanaokosea katika idara nyingine.
Hivyo ameomba wanapogundua kuna askari anaenda kinyume watoe taarifa kwa Mkuu wa polisi wilaya na mkuu wa wilaya badala ya kulaumu jeshi lote, kwani wapo waadilifu wanaofanya kazi vizuri.
Mkuu wa wilaya amehimiza usimamizi wa sheria kuhusu unywaji wa pombe masaa ya kazi na kuwataka polisi kuthibiti wazurulaji na kukomesha tabia ya wananchi wanaoenda kulala uwanjani mchana kwa kuwakamata na kuwaweka rumande wakalale zaidi kama wanasinzia mchana badala ya kufanya kazi.
Maoni
Chapisha Maoni