WALOWEZI 500 KITETO WAANZA KUHAKIKIWA URAIA WAO


WATU 500 KITETO WAANZA KUHAKIKIWA URAIA WAO.

JUMLA ya watu 500 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, wameanza kuhakikiwa uraia wao kufuatia tuhuma za kuishi Nchini kinyume cha Sheria.

Watu hao wanatoka Kata za Kijungu, Sunya na Lengatei ambao waliishi miaka mingi iliyopita kama wahamiaji walowezi.

Kamanda wa Uhamiaji Wilayani Kiteto, Ikomba Eliudi Mathew alisema, sheria ya Uhamiaji Sura ya 54, rejeo la 2016 na kanuni zake imeeleza taratibu za watu kuishi nchini ambao sio raia.

"Sheria ya Uhamiaji sura ya 54, rejeo la 2016 na kanuni zake za mwaka 1997 na marekebisho ya kanuni hizo ya mwaka 2016, raia wa kigeni walioingia nchini kabla ya mwaka 1972 na vizazi vyao kuishi kwa Pasi maalumu ya Kiuhamiaji"

Wakizungumza baada ya uhakiki, watu waliohakikiwa waliomba kutorejeshwa wanakotuhumiwa kufuatia kuishi nchini kwa miaka mingi.

Tunaomba hata kama sheria itabaini kuwa sisi sio raia wa Tanzania kufuatia babu zetu kutoka nje ya Nchi tubaki Tanzania kwakuwa tumeishi miaka mingi humu" alisema Omary Musa Monjela wa Lengatei.

Maoni