Wananchi Mbulu wasisitizwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa

Wananchi Mbulu wasisitizwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Na MOHANED HAMAD

Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara Chelestino Mofuga leo 10/6/2018 amewataka wananchi kuwa na vyeti vya kuzaliwa.

Akiongea na wananchi wa kata ya Silaloda alisema, mwaka jana vijana 33 walikosa kujiunga na JKT kutokana na kukosa vyeti vya kuzaliwa. 

Amesisitiza kuwa vyeti vya kuzaliwa vinahitajika sehemu mbalimbali ambapo wananchi wa mbulu asilimia 95 hawana vyeti vya kuzaliwa. 

Kwa upande wa baadhi ya wananchi walimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuondoa urasimu katika upatikanaji wa vyeti hivyo

"Umaweza kwenda kutafuta cheti cha kuzaliwa, mtu unachukua zaidi ya wiki kufuatilia jambo moja naomba hili jambo lishughulikiwe haraka"

Jafari Hayoda (Mwananchi) alisema vijana wengi wilayani humo wamepoteza nafasi za kazi kwa kutokuwa na vyeti hivyo.

Mkuu huyo wa wilaya alipiga marufuku unywaji wa pombe masaa ya kazi, akisema pombe zinywewe saa tisa alasiri na atakayepatikana kuuza na 

Maoni