Serikali yaipa Mafia Tsh 500 mil kwa shughuli za maendeleo


Mbunge wa Mafia Mhe. Mbaraka Dau


Sera ya Nchi  ya Tanzania, inataka kila Kijiji kuwa na Kituo Cha Afya, lakini hali hiyo ni tofauti  na Wilaya ya Mafia Ambapo Imekuwa  ikikabiliwa na changamoto za huduma  ya  Afya  Kwa Kukosa Kituo Cha Afya hata Kimoja Katika kata 8 zilizopo Wilayani hapo.

Mbunge wa Mafia Mhe. Mbaraka Dau, ameipongeza Serikali ya Awamu ya tano Kwa kuiwezesha Wilaya ya Mafia Kupata Kiasi Cha shilingi bilioni 22 Ambazo titatumika katika Miradi ya Maendeleo Wilayani Humo.

Akizungumza na wakazi wa Kijiji Cha Bweni katika Mkutano wa hadhara, Mhe. Dau amesema Serikali ya awamu ya tano Imetoa kiasi cha Shilingi Milioni  500 Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Kituo Cha Afya Katika Kata Ya kilonge.

Kituo hicho Kitakuwa na uwezo wa kutoa huduma za Mama na Mtoto, Upasuaji na Chumba Maaluma Cha kujifungulia kwa  ajili ya akina mama wajawazito.

‘’Hospitari yetu ya Wilaya imekuwa katika changamoto nyingi  Sana yakini pia Serikali ya Rais Magufuli Imetupatia kiasi cha shilingi 400  mil Kwa ajili ya ukarabati wa ambao unaendea hivi Sasa’’ Alisema Mhe.Dau

Tsh 400 mil zitatumika Kujenga wodi mbili kwa ajili ya wagonjwa wanaotumia Bima ya Afya, ambapo awali Kulikuwa na Changamoto ya kukosekana Wodi maalum ya wagonjwa wanaotumia bima ya Afya na wasio kuwa na bima kupata huduma pamoja hali Iliyokuwa inasababisha usumbufu kwa wananchi.

Aidha Mbunge huyo ametoa Vifaa Mbalimbali Katika Zahanati ya Bweni Iliyokuwa ikikabiliwa na ukosefu wa Vifaa Tiba vya Maabara Pamoja na Madawa na mashuka kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa katika Zahanati hiyo ya Bweni.

Maoni