Askof Chambala afunguka Kiteto

Kiteto. Sauti za wananchi zimepotea, kila wanapozungumza inachukuliwa kama siasa, hali inayofanya kuwa  wawoga wa kusema ukweli na kubaki kusifia viongozi wao kuwa hawaoni kama wanaweza tena kusema jambo la kweli na kusikilizwa na mamlaka zao.

Labda itokee watu waliseme na wasimamia wananchi wasikilizwe kwa kuwa huo ndio msingi wa Dola iliyopo madarakani tofauti na ilivyo sasa wengi wao hawana uelewa wa kutosha juu ya utawala wao.

Akizungumza na Mwananchi leo Aprili 9.2023, Askofu wa Kanisa la Anglina Dayosisi ya Kiteto Isaya Chambala nyumbani kwake baada ya Ibada ya Pasaka amesema, lazima wananchi wasikilizwe kwa kuwa wao ndio chimbuko la uongozi

Mamlaka husika zisimamie haya na watumishi wa umma nao wanatakiwa kuwajibika kwa wananchi kikamilifu tofauti na ilivyo sasa, mwanzo tuliona nidhamu kwa watumishi wa Serikali na baadaye ikapotea…wananchi walithaminiwa sana tu ila sio sasa hivi

“Nikiangalia kabila langu, nachukua na la wenzangu na majirani zangu jinsi tunavyoishi shughuli zetu mambo yetu, utawala uliopita hapo nyuma ulituweka katiia hali flani kuthaminiwa wananchi na watumishi walio madarakani waliwajibika, lakini hali imebadilika”

Alisema kuwa staili za uongozi imebadilika…na uongozi unatofautiana akidai wananchi wanatakiwa kuwa na sauti kwa mamlaka zao, lazima pawe na mtu mmoja wa kuogopewa na watumishi wenzake wa umma ili wawatumikie kikamilifu wananchi

“Kwa kweli nionavyo sauti ya mwananchi sasa imeanza kupoteza hadhi, hawasikiki tena uoga umewatawala kwa sababu hawaoni wakisema watasikilizwa tena, labda itokee tu sasa watu wakusema wananchi wakipiga kelele, wakilalamika wasikilizwe”Alisema Askofu Chambala

Kuhusu suala la Katiba Askofu Chambala alisema Kenya ni nchi marafiki na jirani wa Tanzania wana Katiba nzuri inayowapa wananchi uhuru nafasi…ninaogopa sana kusema lakini je inaodoa matatizo yao? mbona imewafikisha hapo walipo fikia kuwa na mzozo

“Maandamano tunasema ndio haki yamewafikisha Wakenya hapo walipofikia mpaka sasa kwa hiyo naamini katiba mpya ni muhimu Tanzania na itajenga msingi mzuri ni vizuri kuwa nayo lakini kuitekekeza ni jambo lingine” alisema Askofu Chambala wa Kanisa la Anglikana Kiteto

Alisema Katiba peke yake yenye maandishi mazuri haitoshi kuondoa matatizo ya watu lazima ijibu haja za wananchi kama tunavyotaka wananchi, akisema anachoamini Mungu asaidie apatikane mtu mmoja atakayesimamia Katiba hiyo kikamilifu kwa manufaa ya umma ili wananchi waondokana na madhila yanayo wakabili.

Mwisho

Maoni