Karibuni kwenye Blogu yangu upate Matukio Na mambo mbalimbali kila wakati
Aliyelala ni mmoja wa wahanga wa migogoro ya ardhi Bw. Sangali Athumani aliyekatwa mapanga na baadaye kufariki Dunia akiwa Hospitali ya Muhimbili Dar eS Salaam.
Bw. Sangali Athumani wa Kiteto Manyara akiwa amekaa kabla ya kifo chake kilichosababishwa na watu wanaodaiwa kuwa jamii ya kifugaji wamasai kumkata mapanga sehemu mbalimbali za mwili wake
DIWANI AFARIKI KITETO AKICHUNGA MIFUNGO:
Aliyekuwa Diwani wa kata ya Lolela Kone Lembile enzi ya uhai wake akiwasilisha kazi za vikundi katika moja ya Semina mjini Kibaya Picha na Mohd Hamad:
Marehemu Lembile alifariki wakati akikimbizwa kwenda Hospitali ya Wilaya ya Kiteto baada ya kuanguka ghafla akichunga mifugo yake
Kwa mujubu wa Daktari aliyeweza kuuona mwili na kuuchunguza alisema kifi cha Marehemu Lembile kimetokana na presha ya kushuka
Tatizo hilo limemkumba kwa muda mrefu hadi umauti ulipomkuta na kwamba atazikwa katika kata ya Lolela nyumbani kwake siku ya jumatatu.
XXXXXXXXXXX
PICHA YA PAMOJA KWA WANACHAMA WA SHIRIKA LA MWANASATU LINALOFANYA KAZI WILAYANI KITETO
Kiteto
hatutashiriki uchaguzi mkuu 2015
Na Mohamed Hamad
BAADHI ya wananchi wilayani
Kiteto Mkoani Manyara wametishia kutoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2015
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za Serikali kushindwa kuwatambua kwa
kuwakwamua kiuchumi hali inayofafanya waendelee kuwa maskini
Wakizungumza hayo kwenye
mkutano wa katiba ulioandaliwa na Shirika lisilokuwa la Kiserikali la MWANASATO
linalo jishughulisha na utetezi wa wagane na wajane pamoja na makundi maalumu
wamesema hawako tayari kushiriki uchaguzi mpaka Serikali itakapoona umuhimu wao
“Hatuwezi kuitwa makundi
madogo madogo ndani ya jamii wakati tunashiriki kikamilifu kuendeleza nchi hii kwa
kufanya kazi za kuliendeleza taifa lakini mwisho wa siku kupitia IBARA ya 45 ya
rasimu ya katiba ya mwaka 2013 Serikali iseme wakulima na wafugaji ni makundi madogo ambao watatengewa ardhi
kwaajili ya kujipatia risiki”
Wakifafanua Ibara hii
wajumbe hao walisema mameno haya yanaundhi na yanadhalilisha watanzania kuwa
wao Serikali itawapatia sehemi ya ardhi kwaajili ya kujipatia riziki na sio
kuwajengea uwezo kuondokana na umaskini wa kipato
Akizungumza hayo Hasani
Konki (mshiriki) alisema kama katiba ijayo itawatambua wakulima na wafugaji na
kuweka utaratibu maalumu wa kuendesha maisha yao pamoja na kujengewa uwezo wa
kuondokana na umaskiti watashiriki uchaguzi la sivyo hawatakuwa tayarai
Kwa upande wake Kemaa
Lenyirai (mfugaji) alipendekeza katiba ijayo itambue mchango wa viongozi wa
mila ambao wamekuwa msaada mkubwa ndani ya jamii kwa kutatua matatuzo
mbalimbali yanayowahusu
“Kwa mfano jamii ya
kifuagaji hatuna sababu ya kwenda mahakamani tunapohitilafiana badala yake tunawatumia viongozi wa mila kutatua matatizo yetu
kuepuka usumbufu ambao tunauona watu wanapoenda mahakamani ambako rushwa
imekithiri kupata haki”
Kemaa alisema kama Katiba
ijayo itawatambua viongozi wa mila ndani ya jamii ni wazi kuwa matatizo ndani
ya jamii yataisha tofauti na ilivyo sasa kwa kila lalamiko linalowasilishwa
mahakamani kuna ucheleweshaji wa kesi lakini pia kukithiri rushwa
Naye Waziri Godah
(mwanasheria) wilayani humo alilaani kitendo cha tabia za wajumbe wa mabaraza
ya katiba kufanya mzaha katika uchangiaji wa maoni ya katiba mpya akisema wengi
wao wanaingiza mzaha, ushabiki pamoja na dharau
Alisema kama zoezi hilo
litaendelea kuchangiwa kishabiki katiba ijayo haitajibu matatizo ya wananchi na
badala yake itakuwa na mambo machache ambayo itawalazimu watawala kufanya
marekebisha tena kwa siku za usoni
Katika ufafanuzi Godah
alisema wapo watu wanaofika kwenye mkutano kwaajili ya agenda moja tu ya kupiga
kura kutaka aina ya Serikali lakini wamekuwa hawana hoja za msingi kutetea hoja
zao na kuonekana kuwa wameagizwa na watu fulani
Hata hivyo katika zoezi la
kupiga kura juu ya kuhitaji aina gani ya Serikali wanayotaka, idadi kubwa ya
wajumbe hao zaidi ya 80% waalitaka Serikali mbili kwa madai kuwa Nchi ni
maskini haiwezi kuendesha serikali tatu
Mratibu wa shirika hilo
Godwin Nagor akizungumza na BLOG hii baada ya mkutano huo wa katiba alisema wamefikia
wananchi hao kutaka wachangie mapendekezo ya katiba mpya baada ya kutofikiwa na
Serikali
“Shirika tumafanya kazi ya
utetezi wa wagane na wajane pamoja na makundi mengine hivyo baada ya Serikali
kushindwa kuwafikia kama yalivyo makundi mengine Shirika tukaona kuna haja ya
kuwashirikisha kutoa maoni yao”
Alisema ni historia ya pekee
toka kupata uhuru kwa mara ya kwanza Watanzania wanashiriki kuunda katiba yao
tofauti na katiba iiyopita ambazo ilibeba mawazo ya watu wachache na
kusasabisha manunguniko makubwa ndani ya jamii
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni