Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi Jane Mutagurwa akionyeshwa jinsi moto ulivyoteketeza maduka soko kuu ya Kiteto
Maduka kumi yateketea kwa moto Kiteto
Mohamed
Hamad Manyara
ZAIDI ya
maduka kumi ya wafanya biashara wa soko kuu la kiteto Mkoani Manyara yameteketea kwa moto ulioibuka usiku wa kuamkia Aug 23
mwaka huu na kusababisha hasara ambayo thamani halisi haijafahamika kwa haraka
Moto huo
ulianza saa nane za usiku ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya
umeme katika moja ya maduka hayo ambayo yameteketea vibaya baada ya watu
waliofika kushindwa kuudhibiti moto huo
Kwa mujibu
wa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Kibaya Fatuma Ngao amedai kuwa vitu
vilivyoteketea ni pamoja na maduka hayo kumi nyaraka mbalimbali za Serikali ofisi
ya kijiji pamoja na baraza la ardhi la kata
Baadhi ya
mashughuda watukio hili wamezungumza na kipindi hiki na hapa wanasema.. ….
Amsema kuwa
nyaraka hizo ni pamoja na vitabu mbalimbali ambazo zilitumika kama kumbukumbu za
Serikali, viti na meza ambazo zilitumika katika kuihudumia jamii ya Kibaya na
vitongoji vyake
Ngao alisema
alipata taarifa hizo kupitia matangazo yaliyotolewa kwenye moja ya msikiti mkuu
mjini hapo ya kuwaomba wananchi hao ili waweze kufika kuokoa mali zilizokuwa
zinateketea katika soko hilo
Alisema
baada ya wananchi hao kufika walishindwa kuudhibiti moto huo ulioteketeza
maduka yote kwa kuwa hawakuwa na vitendea kazi na kwamba wananchi walilazimika
kuangalia hadi ulipoisha
“Wapo
waliojaribu kutafuta maji kutaka kuzima moto huo lakini walishindwa nguvu na
kuutazama tu hadi TANESCO walipofika na kuzima umeme mji mzima usiku huo lakini
hata hivyo aijasaidia”alisema Ngao
Shuhuda wa
tukio hilo Adiu Ally (mfanya) aliliambia MTANZANIA kuwa baada ya kufika hapo
alikuta kundi kubwa la vibaka wakipora mali mbalimbali sokoni huku wengine
wakijaribu kuzima moto huo
“Nilikimbilia
dukani kwangu na kusimama mlangoni ili vibaka hao wasiibe duka langu lakini maeneo
mengine maduka yaliungua hakuna kilichookolewa huku baadhi watu wakiendelea
kupora vitu mbalimbali vya sokoni”alisema
Katika hatua
hiyo mmoja wa Askari wa kituo cha Polisi kibaya ambaye hakutaka kutajwa majina
yake alisema kuwa duka lake hawakuweza kuambulia chochote baada ya kuteketea
kwa moto huo
Kamanda wa
Polisi mkoani Mnayara Akili Mpwapwa alikiri kuibuka moto huo na kusema kuwa
Jesi la Polisi linaendelea na uchunguzi kutaka kubaini chanzo cha moto huo pamoja
na thamani halisi ya hasara iliyojitokeza
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni