Mtoto aokotwa amekufa kisimani
Na. Mohamed Hamad
MTOTO aliyefahamika kwa jina la Mathias Gwaatema Barani
(8) mkazi wa Kijiji cha Endamanag Kata ya Nar Wilayani Babati Mkoani Manyara, ameokotwa
akiwa amefariki kwenye kisima cha maji kilichochimbwa kwa mikono
Awali mtoto huyo alitumwa kwenda kuchunga mifugo yao na
wazazi wake porini na ilipofika jioni hakuweza kurejea ndipo wazazi wakatoa
taarifa kwa majirani na kuanza safari ya kumtafuta
Akizungumza na BLOG Ofisa Mtendaji wa Kata ya Nar Bw.Phillipo
Moe alisema alipata taarifa kutoka kwa wanajamii hao na baadaye kujulisha Jeshi
la Polisi Wilayani Babati kwaajili ya hatua zaidi
“Binafsi baada ya kupata taarifa niliweza kujiridhisha na
kutoa taarifa Polisi ambapo nao walifika asubuhi ya Leo (jana) na kuelekea eneo
la Tukio ambapo tulimkuta mtoto akielea kwenye kisima cha maji”
Alisema hatua ya kuopoa mwili huo ilifanyika na mwili
kukabidhiwa kwa wazazi wake kwaajili ya mazishi huku Jeshi la Polisi
likiendelea na uchunguzi wa tukio hilo
Ofisa huyo alisema mtoto huyo alitumwa na wazazi wake
kwenda kuchuga mifugo na kuongeza kuwa mifugo ilipatikana siku hiyo na
kurejeshwa nyumbani ikiwe kwenye shamba la mmoja wa wana kijijini hicho
Akizungumzia mazingira ya kifo hicho Mtendaji huyo wa
Kata alisema kuwa hakuna anae hisi chochote juu ya kifo hicho akisema kuwa
huenda mtoto huyo alitumbukia mwenyewe akitaka kunywa maji
“Tunachohisi hadi sasa ni kwamba kwakuwa mtoto huyo
alikuwa ni mdogo labda alishikwa na kiu ya maji na kutaka kuchota maji ili
anywe, kutokana na hatua hizo huenda alishindwa na kudumbukia ndani”alisema
Ofisa huyo
Hata hivyo BLOG ilitaka kujua kama ni kawaida kwa watoto
wadogo kuchunga mifugo katika eneo hilo na kuelezwa kuwa imekuwa ni mazoea kwa
wafugaji kutuma watoto wadogo kwenda kuchunga mifugo
Alisema Serikali imepiga kelele juu ya jamii ya kifugaji
kuacha kuwatumia watoto wadogo kuchunga mifugo bila mafanikio na kuongeza kuwa
tatizo lililopo na ubutu wa sheria ambapo mtu akikutwa na kosa mahakamani
hupewa adhabu ndogo
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Akili Mpwapwa amekiri
kutokea tukio hilo na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi ninaendelea kufanya
uchunguzi juu ya kifo cha mtoto huyo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni