Mwanafunzi Bestina Mchunguzi wa Kiteto Sekondari akiwa katika Hospitali ya
Kiteto baada ya kuchomwa kisu tumboni kwa tuhuma za kugombea wanaume
Mwanafunzi
anusurika kifo kwa tuhuma za mapenzi
·
- Achomwa kisu tumboni,alazwa Hospitali ya Kiteto
Na Mohamed Hamad MANYARA
MWANAFUNZI mmoja wa shule ya Sekondari ya Kiteto
Mkoani Manyara Bestina Mchunguzi, amelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto
baada ya kuchomwa kisu na mwanafunzi mwenzake kwa tuhuma za wivu wa kimapenzi
Akiongea kwa taabu akiwa amelazwa katika Hospitali
hiyo Bestina alisema hali yake bado haijatengemaa kutokana na majeraha
aliyopata ya kuchomwa kisu tumboni pamoja na kukatwa sehemu ya mkono wake
Tukio hilo limetokwa Aug 23 mwaka huu mjini Kibaya
katika viwanja vya shule ya msingi Kibaya ambapo wanafunzi Mwajuma Ally
alimchoma mwenzake kisu tumboni na kumsababishia kutokwa na damu nyingi
hatimaye kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto
Alisema siku hiyo alikuwa mjini Kibaya baada ya
kutoka shule na ndipo walipokutana na mwenzake huyo aliyekuwa na kisu hatimaye
kumchoma tumboni na kuanguka chini
Kwa mujibu wa baadhi ya wanafuzni waliozungumza na
MTANZANIA walieleza kuwa chanzo cha ugonvi huo ni kugombea mabwana ambapo awali
kabla ya tukio walipigana shuleni na waliporejea nyumbani wakaendelea na ugomvi
huo
“Walipigana wakiwa shuleni na walipokutana Mwajuma
alimwambia mwenzake kuwa kwanini ulimitoa damu shuleni akasema leo nitakufanya
nitakavyo, akamchoma kisu tumboni na alipong’ang’ania akakatwa tena
mkononi”alisema mmoja wa wanafunzi hao
Akisisitiza kauli yake hiyo Fatuma Kiteka
(mwanafunzi) alisema kuwa vitendo hivyo vimekithiri shuleni hapo hasa kwa
vijana wa kiume kutoka mitaani kuwa na mahusiana ya kimapenzi na zaidi ya
mwanamke mmoja
“Tunayaona sana hapa shuleni waalimu wamekuwa
wakipiga sana kelele juu ya vitendo hivi lakini wamekuwa wakipuuzwa na leo hii
haya ndiyo madhara yake kwani imekuwa ni mazoea na kama fasheni mwanafunzi kuwa
na bwana shuleni”alisema mwanafunzi huyo
Naye Neema Magimbi (mwanafunzi) alitaja sababu za
wanafunzi kujikita katia vitendo hivyo ni kuendekeza starehe shuleni na wengine
kufanya kazi hizo kama moja ya kujipatia vipato wanapokuwa shuleni
“Wapo wanaofanya kazi hii ili waweze kuishi lakini
pia wapo wanaofanya kwa hulka zao sasa hili sina jibu sana ila tatizo hili ni
kubwa linahitaji nguvu ya ziada hapo shuleni kwa kila mara yanapojitokeza
huishia hewani”alisisitiza Neema
Kwa mujibu wa mmoja wa madaktari katika Hospitali
ya wilaya ya Kiteto ambaye hakutaka kutajwa majina yake alisema hali ya
majeruhi huo inaanza kutengamaa baada ya kusafishwa kidona na kuondeza kuwa
walilazimika kumpiga opereshen ili kumsafisha
Alisema kuwa katika hatua hizo mwanafunzi hiyo
amekazimika kuongezewa damu chupa mbili baada ya kuoneka kuwa na upungufu na
katika hali ya kumwokoa wakalazimika kumwongezea alisema daktari huyo
Uchunguzi uliofanya na MTANZANIA umebaini kuwepo
kwa biashara za ngono kwa wanafunzi hao ambapo mimba na utoro vimetajwa kutokea
katika sekondari hiyo hali inayodaiwa kuwa huwa inazibitiwa mara kwa mara
Akizungumza hayo mwalimu mkuu wa Sekondari hiyo
aliyefahamika kwa jina moja la Kimaro amekiri kutokea vitendo hivyo na kuongeza
kuwa uongozi wa shule hiyo umekuwa macho kuvizibiti na kuongeza hali na
majeruhi huyo inaendelea vizuri
Kuhusu mwanafunzi Mwajuma Ally Mussa kwa sasa
anashikiliwa na Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto kwa Tuhuma za kumchoma mwenzake
na kumsababishia maumivu makali na yuko katika mahabusu ya gereza la Kiteto
Mwanafunzi Mwajuma Ally Musa anayetuhumiwa kumchoma kisu mwanafunzi mwenzake kwa tuhuma za kugombea wanaume
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni