Wanafunzi
32 walala chini kwa miaka mitano shuleni
Na. Mohamed Hamad KITETO
JUMLA ya wanafunzi wa kiume 32 wa shule ya msingi na
ufundi Kibaya iliyoanzishwa mwaka 1950 Wilayani Kiteto Mkoani Manyara,
wanalazimika kulala chini kwa zaidi ya miaka mitano kwa kukosa vitanda.
Akisoma risala kwa mgeni rasmi leo (jana) kwenye mahafali
ya 58 toka kuanzishwa shule hiyo mmoja wa wahitimu hao alitaja changamoto
zinazo wakabili kuwa ni kukosemaka kwa vitanda vya wavulana bweni
Zingine ni upungufu wa viti 39 vilivyopo 11, na meza 37
za waalimu zilizopo 13, vyumba vya madarasa 5 vilivyopo 8, nyumba za walimu 13
zilizopo 6 pamoja na matundu 23 ya vyoo kati ya 6 yaliyopo
Kwa mujibu wa risala iliyosomwa na mmoja wa wahitimu hao
imeeleza kuwa shule hiyo ni ya kutwa na
bweni, ina jumla ya wanafunzi 561 kati ya hao 304 ni wavulana na wasichana 257
“Mheshimiwa mgeni rasmi kwa heshima kubwa na taadhima
mbali na matatizo haya tatizo lingine ni kukosekana kwa uzio hapa shuleni hivyo
watu wanaingia shule kwa muda watakao”
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Bi.Msangi
alieleza MTANZANIA kuwa shule hiyo kwa sasa inakusudiwa kufungwa kwa kukosa
choo chenye hadhi hivyo kuhofiwa wanafunzi kudumbukia
Kwa upande wake Simon Parseko (mwanafunzi) aliwaomba
wadau wa elimu wilayani na nje ya Wilaya kuwasaidia vitanda, magodoro na shuka kwani
wamechoka kulala chini kwa zaidi ya miaka mitano
“Mwalimu alituambia tuwaleze wazazi watununulie vitanda
ili tuje navyo hapa shuleni lakini ilishindikana kutokana na kutojua aina ya
kitanda kinachohitajika hivyo kutulazimu kuendelea kulala chini”
Naye mgeni rasmi Bakari Mahanyu ambaye pia ni mmoja wa
maafisa wa Elimu Wilayani hapo alitupia mpira Serkali ya Kijiji kuwa ndio wenye
jukumu la kufanya ukarabati shuleni unapohitajika
Alisema Serikali imekwisha sogeza huduma karibu na wananchi hivyo wenye jukumu la
kuendeleza shule ni pamoja na wadau wa Elimu, wazazi pamoja na Serikali ya
Kijiji.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni