UKATILI WA KIJINSIA TISHIO KITETO





 Diwani Zamzam Ramadhani Viti maalum CHADEMA akisisitiza jambo kongamano la Jinsia Kiteto

 Mama Nasinyari Lenyirai akisisitiza jambo kwenye kongamano la Jinsia lililoitishwa na Mtandao wa KCS Forum Kiteto

Ukatili wa Kijinsia wakithiri Kiteto

Na Mohamed Hamad
WANANCHI Wilayani Kiteto Mkoani Manayara wameitaka Serikali kuingilia kati na kutokomeza ukatili wa kijinsia uliokithiri na ambao unaleta madhata kwao

Jamii ya kifugaji (wanasai) wametajwa kuwa ni miongoni mwa makabila Wilayani humo yaliyokithiri kwa ukatili wa Kijinsia ambao unatokana na kukumbatia mila potofu

Akizungumza hayo kwenye kongamano la Jinsia lililoandaliwa na mtandao wa mashirika yasiyo ya Kiserikali KCS Forum kwa kushirikiana na (The Foundation for The Civil Society)wilayani hapo Nasinyari Lenyirai (mfugaji) alisema mila potofu zinachangia ukatili ambao sasa ualeta madhara kwao

“Sisi wanawake wa jamii ya kifugaji (kimasai) tunaonekana kama watumwa ndani ya familia zetu na hii inatokana na mila na tamaduni tunazokumbatia”alisema Nasinyari

Alisema mila hizo na tamaduni zinawanyima haki wanawake wengi wa jamii ya kifugaji wamasai na kuongeza kuwa nguvu zaidi zinahitajika kuokoa kundi hilo ambalo linadhulumiwa haki zao kila ukicha

Akitolea mfano wa ukatili wanazofanyiwa kuwa ni pamoja na vipigo, kutofaidi matunda wanayochuma, pamoja na kukosa elimu kwa watoto wao kwa madai kuwa motto akisoma atakosa mahari ya mifugo kuwa hataolewa

Alimtaja mwanamke mmoja aliyefukuzwa nyumbani kwake baada ya kuchuma na mume wake kuwa hakuambulia chochote kutokana na madai kuwa hana haki katika mali hiyo aiyoichumea na mume wake kwa zaidi ya miaka ishirini
Alisema kwa sasa mwanamke huyo anaishi kwa kufanya biashara ya kuuza ugoro soko kuu la Kiteto baada ya kufuatilia haki zake bila mafanikio kutokana na kukithiri kwa vitendo vya rushwa ngazi za maamuzi

Akithibitisha kuwepo kwa ukatili huo mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mainge Ole-Lemalali katika Kongamano hilo alisema bado jamii ya kifugaji wanaume wanamtazamo hasi kwa wenzi wao kuwa hawana haki katika mali

Kutokana na tatizo hilo Mwenyikiti huyo ameahidi kuwa Serikali Wilayani Kiteto itajizatiti kutoa elimu kwa umma kwa kushirikiana na mashirika yasiyo yakiserikali ili kuondoa tatizo hilo

Kwa upande wake Mratibu wa muungano wa mashirika hayo Nemes Iria katika mdahalo huo alieleza kuwa lengo la mdahalo huo ni kuangalia masuala ya kijinsia na changamoto zake

Mwisho

Maoni