Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Minge Lemalali akisisitiza Jambo.
Wananchi
acheni kulalamikia vijiweni
Na. Mohamed Hamad
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mainge
Lemalali amewataka wananchi wilayani humo kuacha utamaduni wa kulalamikia vijiweni
badala yake waende ofisi husika kueleza kero zao
Malalamiko hayo yanatokana na kutoridhika na huduma za
jamii zinazotolewa na Serikali hali inayowafanya wananchi hao kuwa na manung’uniko
na kulalama vijiweni bila kupata ufumbuzi
Akizungumza kwenye kongamano la Jinsia lililoandaliwa na
Mtandao wa Mashirika yasiyo ya Kiserikali (KCS Forum) Wilayani Kiteto
Mwenyekiti huyo alikiri wananchi kutopata huduma za Jamii kwa kiwango stahili
“Wananchi acheni kulalamikia vijiweni kwenye kahawa
njooni ofisini tuongee matatizo yetu ili tuyatafutie ufumbuzi, kwani kuzungumza
vijiweni hakusaidii kufumbua tatizo”alisema Mainge
Alisema yapo matatizo mengi ya ardhi katika mirathi,
huduma za maji, Afya, kuwa kuna changamoto nyingi zanahitaji kuzungumza kwenye
vikao na hata ofisini na sio vijiweni kama ilivyo sasa
Aidha Mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa ili wananchi
waweze kupata maendeleo lazima kuwepo kwa maafikiano ya viongozi katika
kujadili na kufikia mwafaka mambo yanayowahusu
Kwa upande wake Ramadhani Machaku (Zoa) akizungumza na BLOG
kuhusu malalamiko ya wananchi alisema kuwa wananchi wamekosa imani na kukata
tamaa kwa viongozi wao kuwa wanaweza kuwasaidia
Alisema kila mara wamekuwa wakiilalamikia Serikali yao
juu ya huduma mbovu za Afya,Elimu, na hata maji viongozi wanajua lakini
wamejifanya kuwa sehemu ya watu wasiojua kinachoendelea
“Hata huku kuzungumzia vijiweni ni matokeo ya
kutoshughulikiwa malalamiko yetu na huko tunajasirishana ili kutengeneza uelewa
wa pamoja mwisho wa siku tuwe na maamuzi pamoja”
Alisema tatizo la wananchi ni Serikali iliyopo madarakani
kuwahujumu, hivyo hakuna kiongozi asiyejua hitaji lao na hata kama viongozi
wanataka kuzungumza na wananchi ni kujikosha alisema Mwananchi huyo
Ameitaka Serikali kuacha kuruka kimanga juu ya kutojua mahitaji
ya wananchi hasa akisema kuwa,viongozi walipokuwa wanahitaji kuingia madarakani
waliyajua matatizo ya wananchi na sio vinginevyo
Naye mratibu wa mtandao wa mashirika yasiyokuwa ya
kiserikaili KCS Forum Nemes Iria akizungumza kwenye kongamano hilo la Jinsia
alisema lengo la mashirika ya umma ni kuisaidia Serikali katika majukumu yake
Alisema yapo matatizo mengi yanayo wakabili wananchi akidai
kuwa mengi ni yakisera zaidi ambayo wakati mwingine Serikali inatakiwa
kurekebisha baadhi ya Sheria zinazowakandamiza wananchi
Mmoja wa wanajamii ya kifgaji wmasai akijaribi kupitia Rasimu ya katiba
Maoni
Chapisha Maoni