MADIWANI KITETO WAMKATAA MKURUGENZI MBELE YA RC

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akisisitiza jambo kwenye kikao cha madiwani Kiteto kulia ni Mkuu wa Wilaya y kiteto Bi. Martha Umbulla kusoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri Minge Lemalali

Madiwani wamkataa DED Kiteto mbele ya RC

Na Mohamed Hamad MANYARA 0707 055080
MADIWANI wa Halamashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara kwa kauli moja wamemkataa Mkurugenzi wao wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Jane Mutagurwa wakidai kutoridhiwa na utendaji wake wa kazi

Uamuzi huo umefikiwa leo (jana) mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo kwenye kikao cha baraza maalumu la madiwani kilichoketi kujadili hoja za ukaguzi ambapo Halmashauri hiyo imepata hati yenye mashaka kwa miaka mitatu mfululizo

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara juu ya ukaguzi wa mdhibiti wa hesabu za Serikali imeeleza kuwa Halmashauri hiyo imeporomoka kwa kiwango cha usimamizi wa fedha na kupata hati yenye mashaka kwa miaka mitatu mfululizo

Ilielezwa hadi kufikia 2011/2012 halmashauri ilikuwa na hoja 52 ambapo hadi Sept 2013 jumla ya hoja hizo zilikuwa hazikufungwa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo udhaifu wa madiwani kushindwa kuwajibika katika nafasi zao

“Mhe Mwenyekiti napenda kuonyesha mbele yako kuwa sikuridhishwa na mwenendo wa usimamizi wa fedha katika Halmashauri yako,ambapo kwa mjibu wa taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa Hesabu za Serikali 2011/2012 Halmashauri hii pekee Mkoani Manyara ndio iliyopata hati yenye mashaka”

Aidha yamatajwa maeneo makuu yenye udhaifu katika taarifa hiyo kuwa ni malipo yenye nyaraka pungufu Tsh mil 7,211,499,.99,manunuzi ya shajala ambayo hayajathibitishwa mil 22,832,083

Mengine ni maduhuliyaliyokusanywa na mawakala ambayo hayakupelekwa Benki Tsh mil 513,613,560,maduhuli ambayo hayakupelekwa benki na mhasibu wa mapato mil99,516,950, vitabu 44vya kukusanya maduhuli ambavyo havikuonekana wakati wa ukaguzi pamoja na mitambo yenye thamani ya Tsh mil101,246,853.40

Katika hitimisho la mkuu hiyo wa mkoa wa Manyara alisema kuwa hoja hizo zimetokana na uongozi na manejimenti ya Halmashauri kuwa dhaifuna kutokuwa makini katika ukusanyaji wa mapat,utunzaji wa nyaraka,usimamizi wa mikataba,na kutowajibika kwa watumishi  watumishi

Hata hiyo taarifa hiyo iliwachefua madiwani hao wakisema udhaifu huo hautokana na wao badi tatizo liko kwa mkurugenzi mtendaji ambaye kilammara amekuwa akipuuzia ushauri wa madiwani katika kuiendesha Halmashairi hiyo

Akionyesha hisia zake Mohamed Benzi (CCM) Diwani wa Dosidosi alisema haoni sababu ya ya kulaumiwa madiwani na badala yake lawama hizo zielekezwe kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Bi. Jane Mutagurwa

Wakati Mkurugenzi huyo akitupiwa madongo hayo hakuwepo na kaimu wake Emanuel Mwagala alilazimika kupokea na kudai kuwa ataenda kumweleza kilichozungumzwa kwenye kikao hicho maalumu kujadili hoja za ukaguzi
Akijibu baadhi ya hoja zilizokuwa zinatakiwa kutolewa maelezo Nassoro Mkwenda alitakiwa kutotetea kilichoambiwa kuwa ni uongo kwa madai kuwa hakuwepo katika kipindi hicho na kutolewa taarifa kuwa ifikapo tar 15 Dec hoja hizo ziwe zimejibiwa kikamilifu na Mkuu wa mkoa atafika kwaajili ya kujiridhisha na majibu hayo

Hata hivyo Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa Serikali imeanza uchukuwa hatua dhidi ya watumishi wasio waadilifu ambapo baadhi yao wamehamishwa na kwenda maeneo mengine kikazi kutokana na kutowajibika kwao

Miongoni mwa watumishi waliohamishwa ni pamoja na Afisa mipango Mageza,Mweka hazina wa Wilaya pamoja na Mkaguzi wa ndani ambao wote kwa kipindi hicho walikuwepo na sasa hapo na kuletwa wengine kufanya kazi wilayani hapo

Wakati akitoa taarifa hiyo baadhi ya madiwani walisikika na kumtaka mkuu wa mkoa kuondoka na Mkurugeni Mtendaji Bi. Jane Mutagurwa ambaye naye ameshindwa kuwasaidia kwa kipindi chote alichokuwepo na kudai kuwa hawako tayari kushirikiana nao

Mkuu wa Mkoa katika kauli hiyo alisema mbele ya kikao hicho kuwa amesikia na atafanyia kazi taarifa hiyo ambayo nae imemsikitisha kuona mambo yakiharibika kwa miaka mitatu mfululizo akisema Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto imnatia doa Mkoa wa Manyara

Mwisho  

Maoni