DED KITETO APEWA SIKU 30 KUSAFISHA MJI WA KIBAYA

DED KITETO APEWA SIKU 30 KUSAFISHA MJI WA KIBAYA

Na Mohamed Hamad
BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara
limempa siku 30 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi. Jane
Mutagurwa kuhakikisha kuwa lori la kubebea taka linapatikana katika
mji wa Kibaya

Hatua hiyo imefikiwa na madiwani hao mwishoni mwa wiki baada ya kuwepo
kwa madai ya kukithiri kwa uchafu katika mji wa Kibaya ambako ndio ni
makao makuu ya Wilaya ya Kiteto yaliyopo na kuhofiwa kuwa huenda
magonjwa ya mlipuko yakaibuka

“Mhe.Mwenyekiti,tusisubiri mpaka wananchi waandamae ndio tutoe huduma,
hakuna asiyefahamu kuwa mji wa Kibaya umekithir kwa uchafu sasa
wananchi wanatuangalia sisi kama wawakilishi wao kwanini tusubiri
mpaka waandamane?”

Akizungumza kwa hisia kali Leonard Kunamila Diwani wa kata ya Engusero
(CCM) alisema watendaji kushindwa kuwajibika katika nafasi zao
kunachangia wananchi kuichukia Serikali yao akisema wenye kulaumiwa
hasa ni wanasiasa na Serikali yao

Naye Simon Mbaiyo Diwani (CCM) kata ya Ndedo amliwaomba madiwani
kumuunga mkono akitaka Mkurugenzi ndani ya siku siku 30 awe
ametengeneza lori akisema kuwa ni aibu kwa Wilaya kama Kiteto kukosa
lori

“Haingii akilini hata kidogo Wilaya yenye rasilimali nyingi kama hii
kukosa lori,ni uzembe wa hali ya juu,naomba mniunge mkoni madiwani
wenzangu kwani kama kila mtu atawajibika katika nafasi yake tunaweza
kuwapatia wananchi huduma bora”alisema Mbaiyo

Mwenyekiti wa Halmashairi ya Wilaya ya Kiteto Mainge Lemalali katika
ombi hilo aliunga mkono hoja hiyo pamoja  akisema suala la uwajibikaji
wa watumishi wa Halmashauri Serikali linasuasua na kuwatishia
kuwafukuza kazi

Kwa upande wake Inocent Munga kwa niaba ya Bwana Afya wa Wilaya
alisema tatizo lililopo ni Halmashauri kushindwa kumlipa mzabuni ambae
kwa zaidi ya miezi mtitatu amekuwa akiidai Halamshauri kwa kazi
aliyofanya

Sitaki kuwa msemaji wa Hili hata mkurugenzi mwenyewe anafahamu wakati
mwingine tumelazimika kutoa hata hela zetu mfukoni kulinda kazi kuzoa
taka lakini kwa sasa hali inazidi kuwa mbaya taka ni nyingi na hakuna
wa kuzizoa

Kwa mujibu wa mzabuni wa kufanya usafi katika mji wa Kibaya alisema
kuwa anashindwa kuendelea kufanya kazi kwakuwa nae anadaiwa na
wafanyakazi wake ambao kwa sasa wamegoma kufanya kazi

Mwisho

Maoni