MANYARA YAPATA MIL 48 TOKA UTPC

MAMEC yapata mil 48 toka UTPC. Na Mohamed Hamad MANYARA. Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Manyara (MAMEC) imeupongeza muungano wa klabu za Waandishi hapa nchini UTPC, kwa kuwafadhili zaidi ya Tsh. 48,628,000 pamoja na vitendea kazi mbalimbali kwa waandishi hao. Mwenyekiti Benny Mwaipaja wa Klabu hiyo alitoa shukurani hizo mjini Babati kwenye kikao cha kamati ya Utendaji, akisema umoja huyo umekuwa msaada mkubwa kwa Klabu yake na hata vilabu vingine hapa nchini “Vifaa tulivyopokea ni nguzo muhimu katika utendaji kazi wa kila siku wa Waandishi wa habari,hivyo hatuna budi kuwashukuru na kwa sasa naamini hakuna mwaandishi Mkoani Manyara atakaeshindwa kufanya kazi” “Hakutakuwa na kisingizio cha kushindwa kufanya kazi wakati wowote mara mwandishi apatapo habari,hivyo kwa msaada huo ni wakati mwafaka kwa sasa ambao awali waandishi walishindwa kupeleka habari kwa wakati”alisema Mwaipaja Katika msaada huo Mwenyekiti huyo alitaja baadhi ya vifaa walivyopokea hivi katibuni kuwa ni pamoja komputa tano mpya,laptop mbili,printa mbili,projekta mbili, video kamera moja ya kisasa,tv set moja, Redio,kamera mbili zapicha za mnato na voice recoda. Alisema kwa kupata vifaa hivyo ni dhahiri kuwa hakuna mwandishi atakayelalamila kushindwa kufanya kaz na kuwataka kuwa huru kuvitumia kwa umakini ili viweze kutumika kwa muda mrefu na kwa lengo lililokusudiwa cha Umoja huo Amewataka waandishi hao kutumia fursa hiyo iliyopo adhibu ambayo awali haikuwepo na kuongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa bahati hii isiweze kujirudia na kusisitiza kila mtu aweze kujitambua katika nafasi yake Aidha amedai kuwa MAMEC ina malengo makubwa kwa wanachama wake katika kuhakikisha kuwa wanapata yale wanayotakuwa kuyapana akisisitiza kuwa siri ya mafanikio ni NIDHAMU pamoja na uwajibikaji katika kazi hizo Hata hiyo Klabu ya waandishi wa habari mbali na vifaa hivyo pia waandishi wake wamejengewa uwezo wa mafuzo mbalimbali ambayo yamekuwa msaada wakati wa kufanya kazi zao za kila siku za kiuandishi Baadhi ya mafunzo hayo Mwenyekiti huyo aliyataja kuwa ni pamoja na mafunzo ya kuandika habari za mahakamani,ufuatiliaji wa bajeti,Haki za Binadamu,Habari za vijijini,pamoja na habari za uchunguzi Mwisho.

Maoni