UFISADI MKUBWA WADAIWA KUTOKEA OPERESHENI YA EMBOLEY MURTANGOS
NA.MOHAMED HAMAD
OPERESHENI ondoa wakulima na wafugaji katika eneo la Emboley Murtangos
Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, imesitishwa ghafla kuhofia maafa
ambayo yangeweza kujitokeza kati ya wakulima na wafugaji wakigombea
ardhi
Hatua hiyo imefikiwa na uongozi wa Taifa kuingilia kati kunusuru hatua
iliyofikiwa na uongozi wa Wilaya na Mkoa wa Manyaea ya kuwaondoa
wakulima na wafugaji waliopo katika eneo hilo kwa nguvu kwa madai
wanafanya uharibifu wa mazingira
“Ni kweli tulianza Operesheni ya siku saba kutaka kuwaondoa wakulima
na wafugaji waliopo maeneo ya Emboley Murtangos kwa kutumia kikosi cha
Askari Polisi, ambapo kwa hatua ya awali tulianza kuwapa taarifa kwa
njia ya Spika”
“Na baada ya matangazo kilichokuwa kinafuata ni kutumia nguvu kuvunja
makazi ya wananchi kwa watakao kaidi kwa lengo ya kurejesha eneo hilo
katika hali yake ya mwanzo”alisema Mkurugenzi Mtendaji
Huwezi kutumia nguvu bila kuwapa taarifa wananchi hao kuwaondoka
pamoja na kwamba hawako kihalali katika maeneo hayo (wavamizi)
tulisema tufuate taratibu zote za kisheria watakaokaidi sheria ifuate
mkondo wake alisema Mutagurwa
Habari za uhakika zilizofikia RAI zimesema kikosi cha Askari Polisi
kilipata upinzani mkali katika aeneo hayo wakati wa kutoa matangazo
baada ya kutupiwa mawe na mishale na baadhi ya wananchi wanaoishi humo
Hofu ya mauaji imekuja baada ya wakulima na wafugaji kutishiana,wakati
wakulima wakigoma kuondoka wakidai kuwa maeneo hayo ni yao wafugaji
wamedai watatumia walinzi wa jadi kuwaondoa wakulima katika maeneo
hayo
Zoezi hilo limeonekana kuratibiwa na kundi la wafugaji (wamasai)
kuchanga mifugo na fedha kwa kusimamiwa na Halmashauri, kwaajili ya
kuwezesha shughuli za kuvunja makazi ya wakulima katika eneo hilo kwa
madai ya kuharibu mazingira
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za uhakika zimeeleza kuwa ndani ya
siku tano kuanzia tarehe 08.11.2013 hadi 12.11.2013 jumla ya tsh mil
68,792,850.00 zimedaiwa kutumika kwaajili ya vikao vya maandalizi ya
hamasa za uchangishaji
Pia fedha zingine ni kwaajili ya chakula cha Askari wa kwenye
operesheni,posho zao,pamoja na posho za wajumbe walioshiriki katika
vikao mbalimbali vya kuandaa kufanikisha zoezi la uchangishaji wa
fedha hizo
Mbali na fedha hizo, hivi karibuni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
Mainge Ole-Lemalali alisema kuwa zaidi ya tsh mil 700 zimetumika
katika zoezi hilo mwaka jana kuwaondoa wakulima akisema safari hii
wakulima wataondoka kwa gharama yoyote
Kwa mujibu wa barua ya Mkurugezi aliyoandikia vijiji 58 vya Kiteto
alitaka kila kijiji kichange mil 20 kwaajili ya kulinda msitu huo
akisema kama mchango huo utafanikiwa Wilaya itaepuka kupata jangwa
kutokana na kasi ya uharibifu wa mazingira uliopo
mwisho

Maoni
Chapisha Maoni