DC Kiteto
aaswa kutowaondoa wakulima kabla kesi kumalizika
NA.MOHAMED HAMAD
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara Martha Umbulla
ameaswa kuacha kuwaondoa wakulima 50 waliofungua kesi dhidi ya Halamshauri
katika eneo linalogombaniwa la Emboley Murtangos kuwa waachwe kwa kuwa kesi iko
mahakamani
Kesi iko mahakama ya Rufaa yenye namba 140/2012,
imepangwa kusikilizwa Feb 13 mwaka huu kwamba hivi karibuni Mkuu wa Wilaya alitoa
amri kuwataka watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu
kilimo,ufugaji,na uchomaji mkaa watoke kuwa waachwe mpaka kesi imalizike
Jumla ya wakulima 50 wakiongozwa na Tito Shumu walifungua
kesi ya msingi kupinga amri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kuvunja makazi
yao kwa madai kuwa wamevamia na kuanzisha vitongoji haramu kwa kufanya shughuli
za kilimo
Kwa mujibu wa barua ya Wakili G. S. OKWONG’A anaye
watetea wakulima ya Jan 23 mwaka huu kwa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto kupitia amri
yake ya Jan 21 .2014 kuwataka wakulima hao kuondoka ameombwa kusitisha kutokana
na kuwepo kesi inayoendelea mahakama ya Rufaa Dar
“Mheshimiwa
kwa kuwa kuna kesi ya msingi Mahakama ya Rifaa na imepangwa kusikilizwa tarehe
13/2/2014 tunakuomba utumie busara zako kusitisha amri ya kuwaondoa wateja wetu
katika eneo lenye mgogoro mpaka hapo kesi itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi”ilisema
sehemu ya barua hiyo
Hata hivyo pamoja na taarifa hiyo ya kimaandishi kwa Mkuu
huyo wa Wilaya pia alipatiwa viambatanisho vya vivuli vya wito wa Mahakama na
pia hoja ya maandishi aliyoitoa ya kuwataka watu wote waliopo katika eneo la
Emboley Murtangos waondoke mara moja
“Watu wote wanaoishi na kufanya shughuli za kibinadamu,
hususani kilimo,ufugaji,uchomaji wa mkaa katika eneo lote la Hifadhi ya Emboley
Murtangos muondoke mara moja kulingana na amri iliyotolewa na Mahakama ya Rufaa
Tanzania mwaka 2012”
“Kwa mujibu wa mamlaka niliyopewa mnatakiwa muondoke wote
ndani ya siku mbili kuanzia Jan 21-23
mwaka huu,yeyote atakayekaidi amri hii atachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa kosa la kutokutii amri halali
ya mahakama”ilieleza amri hiyo ya Mkuu wa Wilaya
Amri hiyo imekuwa ikitolewa na baadhi ya viongozi
mbalimbali wa Wilaya, Mkoa,na hata Taifa kuwa pamoja na kufahamu suala hili
liko mahakamani, wamekuwa wakiwahadaa wananchi na kuwapa usumbufu uliodaiwa
kuleta madhara makubwa kwao
Jan 16 mwaka huu Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyewasili
Wilayani Kiteto kutoa pole kutokana na maafa ya watu 10 yaliyofanywa na kikundi
cha watu wachache kwa maslahi yao binafsi ambapo aliagiza wakamatwe mara moja na
kufikishwa mahakamani
Jumla ya watu 35 walikamatwa na Polisi, 12 walifikishwa
mahakamani na kufunguliwa kesi ya mauaji, 10 wako chini ya uangalizi wa Jeshi
la Polisi,7 waliachiwa huru baada ya
Polisi kujiridhisha na wengine 6 wanaendelea kuhojiwa juu ya mauaji ya watu 10
Jan 12 mwaka huu katika vitongoji vya Kwa Mtanzania na Laitime Wilayani humo.
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni