MAUAJI KITETO YAZIDI KUJITOKEZA SERIKALI VUNJENI UKIMYA
Wakulima
10 wauawa kwa kuchomwa mikuki Kiteto
·
-Ni Mwendelezo wa mauaji Wilayani kiteto
·
OCD awahi eneo la tukio kuzima mapigano
·
RC Manyara akiri madudu Kiteto
Na. MOHAMED HAMAD
WAKULIMA sita wa kijiji cha Namelock Kata ya Namelock
Wilayani Kiteto Mkoani Manyara wameuawa kwa kuchomwa mikuki sehemu mbalimbali za
miili yao baada ya kuvamiwa kwenye makazi yao na kundi kubwa la wafugaji
(wamasai) wakiwa na silaha za moto bunduki, mikuki, sime, na marungu
Vifo hivi ni mwendelezo wa mauaji yanayofanywa na jamii
ya kifugaji (wamasai) ikielezwa kuwa miili mingine iko porini wakilenga
kuwaondoa wakulima kwa nguvu baada ya madai yao kuwa Halamshauri imeshindwa
kuwatoa wakulima hao katika maeneo yao
Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Akili
Mpwapwa amethibitisha kutokea vifi hivyo akisema miili mingine inayodaiwa kuwa
porini inasakwa kutokana na jamii ya wafugaji wamasai kuvamia wakulima katika
maeneo yao
“Ni kweli kuna idadi ya watu sita waliopotea maisha na
majina yao hayajafahamika mapema kuwa wameuawa na wafugaji katika maeneo ya
laitimi wakiwa mshambani huu ni mwendelezo wa migogoro ya ardhi Wilayani Kiteto
kati ya wakulima na wafugaji” alisema RPC
“Halmashauri ilituchangisha mamilioni ya fedha kwaajili
ya kuwaondoa wakulima, ikiwa zoezi hili likisimamiwa na mkurugenzi kwa
kushirikiana na viongozi wa mila wa jamii ya Kimaai ili kupata fedha
zitakaosaidia mamlaka inaohusika kuwatoa kwa nguvu kotibroka na
(Polisi)”alisema mmoja wa wafugaji
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Eraston Mbwillo
Kisioki Mesiaya (mfugaji) Jan 9 alisema wamasai wamechangishwa mamilioni ya
fedha na Mkurugenzi kwa madai ya kuwaondoa wakulima, kwa kuwa kazi hiyo
haikufanywa na Halamshauri wafugaji wao wameamua kuifanya
Kwa mujibu wa Diwani wa kata ya Sunya Mussa Briton
alisema watu wawili wamepoteza maisha na wengine zaidi wamedaiwa kutoonekana kwenye
makazi yao baada ya kuvamiwa wakiwa eneo la Lemenye na Laitimi ambako hufanya shughuli zao
za kilimo
Alisema Mauaji hayo ni ya maksudi yanayotekelezwa na
jamii ya kifugaji wamasai akidai kuwa, pamoja na kutajwa majina ya baadhi ya
watu wanaopanga njama hizi imeshindikana kukamatwa kwa madai kuna mkonno wa
kiongozi wa Wilaya anaye wasimamia
“Haiwezekani hata kidogo watu wafanye mauaji na kutajwe
wasikamatwe kwa madai eti wanamahusiano na kiongozi wa ngazi ya juu ya juu,
jambo hili halikubaliki naomba Serikali ya ngazi ya Taifa kuingilia
kati”alisema Beriton
Alisema jamii ya Kifugaji wamasai wamekuwa wakiwavamia
wakulima na kuwaaua kisha kukimbilia porini na baada ya muda hurejea na
kuwavamia tena akidai kuwa tukio hili ni la nne toa Dec 21 hadi Jan 12 mwaka
huu kuwa zaidi ya watu kumi wamepoteza maisha
Kwa upandw wao wakulima wamedai kuwa wako tayari kuuawa
ili Serikali iingilie kati wakidai kuwa nayo imechangia kwa kuwagawa wakulima
na wafugaji Kiteto kikabila na kuendekeza Rushwa iliyokithiri na kusababisha
madhara makubwa
“Serikali inajua kuwa ilifanya nini mpaka sasa mauaji
yanatokea watakaobaki wataeleza kilichotuua sisi kwani Serikali ya Kiteto
inahusika katika mauaji haya kwani imekula feda za wafugaji na inashindwa
kurejesha”Alisema Bakari Maunganya Mkulima
Baadhi ya wananchi Wilayani humo wameutupia lawama
uongozi wao wa Wilaya akiwemo Mbunge wao Benedict Ole Nangoro kwa kutoshtuka na
mauaji ya kinyama yanayoendelea kujitokeza Jimbo kwake wakisema kuwa huenda
anahusika
Akiuliza swali Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Saidi
Mwawa alimtaka Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Umbula kueleza umma kuwa Mbunge wao
yuko wapi na kuelezwa ana kazi maalumu aliyopewa na Mh. Rais hivyo asingweza
kufika kwenye mkutano huo
Kwa mujibu wa taarifa za uhakika zimeeleza kuwa chanzo za
mapigano hayo ni jamii ya kifugaji kuchangishwa fedha na uongozi wa Halmashauri
ili waweze kuwaondoa wakulima wapate maeneo ya malisho
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa manyara Eraston Mbwillo
amekiri wafugaji kuchangishwa fedha kinyume na taratibu za Kiserikali akisema
kuwa atahakikisha kuwa waliohusika na suala hili sheria itafiata mkondo wake
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto
Bi. Jane Mutagurwa alikiri kuchanga fedha hizo akidai kuwa waliohusika kuchanga
ni jamii ya watu wa Kiteto kwaajili ya kuisaidia Halmashauri kwenye operesheni
ya kuwaondoa wakulima katika hifadhi
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni