Halamshauri
Kiteto kuburutwa Mahakamani
·
- Ni baada ya kuvunja makazi ya wakulima
Na. Mohammedi Chumvi
JUMLA ya wakulima 20 wa Kijiji cha Kimana Wilayani Kiteto
Mkoani Manyara wameapa kuishitaki Halmshauri ya Wilaya ya Kiteto kwa madai ya
kuvunjiwa makazi yao kinyume na sheria na kusababishia hasara ya zaidi ya
million thelathini na tano
Makazi ya wakulima hao yalivunjwa kutokana na operesheni
maalumu iliyofanywa na Halmashauri aya Wilaya na kudaiwa wakulima waliporwa
fedha,simu za mikononi,pamoja na mali mbalimbali za dukani
“Binafsi nyumba yangu ilivunja kulikuwa na duka lililokuwa
limesheheni vitu mbalimbali ikiwemo sukaru unga wa ngano n vitu vingine ambapo Askari
Polisi na Migambo wakiongozwa na OCD walivamia na kuvunja nyumba pamoja na
kuchukua fedha taslimu zaidi ya mili 9 za kulipa vibarua”alisema Vita bado
(mkulima)
Katika hatua nyingine mkulima huyo alisema kama kweli kulikuwa
na uhalali ya zoezi hilo alipaswa kukamatwa akiwa na vifaa hivyo na kufikishwa
mahakamani kwa kuwa siku zote yupo na ameendelea kupata vitisho vya maisha akiwempo
humo
Kwa upande wake Mntunte Waziri (mkulima) akizungumza na
NIPASHE alisema amesababishiwa hasara ya zaidi ya mil 15 baada ya kikosi hicho
kuvamia kwake na kuchoma moto nyumba zake tatu zikiwa na fedha zaidi ya mil 9
zilizokuwa ndani pamoja na vitu mbalimbali zikiwemo nguo na thamani zingine
“Ninachofanya ni kuwasiliana na wezangu ambao kwa pamoja
tumeamua kuishitaki
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto walioamua kutufilisi ili
Sheria ifuate Mkondo wake kwani tumedhalilishwa sana,tumenyanyasika na familia
ndani ya nchi yetu kwa ujumla”alisema Mntunte
Naye Ibrahimu Msindo (mkulima) alisema Halamshauri ya
Wilaya ya Kiteto inafanya kazi kimila kwa kuamuriwa kufanya kama watakavyo
wafugaji akisema kuwa walichanga zaidi ya mil 500 ili kuwatoa wakulima
“Kimana haipo kwenye nakala ya hukumu iliyotaka wakulima
na wafugaji waliopo humo waondolewe tena kwa kupewa elimu na sio kuvunjiwa kama
walivyofanya Halamshauri sasa hapa lazima tuingie mahakamani”alisema Msingo
Wakati Halmashauri ya Wilaya ikiwa katika Operesheni ya
kuwatoa wakulima waliopo kwenye eneo la Hifadhi ya Emboley Murtangos wafugaji
wamedaiwa kutumia fursa hiyo kuchunga mifugo yao kwenye ashamba ya wakulima
Akizungumza hayo Bakari Maunganya (Mkulima) alisema jamii
ya kifugaji wamasai wamekuwa kama Serikali Wilayani Kiteto akisema Viongozi wa
Kiteto wanafanya kama wanavyotaka wafugaji mfano kuwatoa wakulima li wachunge
mifugo yao
Hivi karibuni Kisioki Mesiaya (mfugaji) akizungumza mbele
ya mkuu wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo alisema wafugaji walichangishwa na
Uongozi wa Halamshauri ya Kiteto ili waweze kuwapatia maeneo ya kuchungia
mifugo yao
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Bi. MARTHA Umbula akizungumza na
NIPASHE Ofisini kweke alisema kutokana na zoezi hili hakuna mkulima wala
mfugaji aliyopo kwenye eneo la Hifadhi hiyo na kwamba Serikali inatekeleza
agizo la Mahakama kuu kuwa eneo hilo pasifanyike shuguli za kibinadamu
Kuhusu mifugo kuchunga
mashamba ya wakulima Mkuu huyo wa Wilaya alisema hata yeye amesikia hilo
akisema kitendo hicho ni kosa kwa wafugaji na kuwataka waache kitendo hicho
mara moja
Kuhusu kuvunjwa kwa makazi ya baadhi ya wanakijiji wa
Kimana alisema kama kweli hawapo kwenye eneo la Emboley Murtangos Serikali
itawagharamia hasara iliyopatikana akisema kuwa kweli kuna mpaka uliowekwa mpya
na kuongeza eneo hilo akisema upo utaratibu unaoandaliwa
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni