MADIWANI KITETO WAGAWANYIKA UJENZI WA SOKU KUU LA KIBAYA

 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Jane Mutagurwa akikagua soko kuu ya Kibaya baada ya kuungua mwishoni mwa 2013

Madiwani Kiteto wavutana kuhusu ujenzi soko la Kibaya

NA. MOHAMED HAMAD
Madiwani wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Mkoani Manyara wamejikuta katika wakati mgumu kwenye mjadala wa ujenzi wa Soko la Kibaya lililoungua mwishoni mwa mwaka jana baada ya kila mmoja kutaka hoja yake izingatiwe

Kaimu Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto Rajabu Chongoe alisema Halamshauri ya Wilaya imetenga mil 100 katika Bajeti yake kwa mwaka 2014/2015 kati ya mil 400 zinazohitajika kukamilisha soko  hilo

“Wahemiwa pamoja na uhitaji soko la Kibaya kwa sasa kama lilivyokuwa linatumika, Bajeti ya mwaka huu tumetenga kiasi cha mil 100 ambazo tungepata Baraka kutoka kwenu zingeweza kuanza kazi mara tu baada ya kuzipata kutoka Serikali kuu”

Wakati hayo yakielezwa hoja zilianza kwa madiwani wakisema hicho ni kidodo huku wengine wakidai kielekezwe kwenye soko la Sunya ambalo limetelekezwa kwa muda mrefu na wengine kudai soko hilo lisijengwe hapo kutokana  eneo hilo kuwa dogo

Hassani Benzi (CCM) Diwani wa Dosidosi akichangia hoja hiyo alipendekeza kuwa litafutwe eneo linguine kuajili ya ujenzi huo kutokana na kukua kwa mji na kwamba Soko linalotakiwa kujengwa ni la kisasa na ambalo litakidhi vigezo vya masoko makubwa hapa nchini

“Sioni sababu ya kuwa na soko dogo hapo linalohitajika la kisasa zaidi tofauti na lililokuwemo awali kwani lazima liwe na miundombinu ya kukabiliana na majanga ya moto na kadhalika na sio kama lile lililoungua”alisema Benzi

Nae Mussa Britoni (CCM) Diwani wa Sunya alisema kutokana na kutengwa kiasi kidogo cha fedha hizo hazitoshi hivyo zielekezwe kwenye kata yake ambako kuna soko la muda mrefu lililotelekezwa na halijakamilika ili zisaidie wananchi hao

Kwa Upande wake Mwasigwa Kimosa  aliwataka wataalamu kutafuta eneo mbadala katika mji wa Kibaya ambalo fedha hizo zitaelekezwa hapo kwaajili ya ujenzi wa awali ili mwaka mwingine watenge kiasi kingine cha fedha kukamuilisha Soko hilo

Hadi hoja hiyo inafungwa hakuna jibu la moja kwa moja lililopatikana  kuhusu hatma ya soko hilo na kwamba wafanya biashara hao wamebaki njia panda kwa kutojua lini soko hilo litajengwa na wapi ili waweze kuendelea na biashara zao

Hata hivyo Mainge Lemalali Mwenyekiti wa Halamshauri ya Wilaya ya Kiteto akihitimisha hoja hiyo alisema kiasi hicho ni kidogo na tegemeo la Halamshauri ni kupata fedha kutoka Serikali Kuu ambao nao huchelewa kutoa

“Fedha nyingi ni kutoka kwa wafadhili ni mpaka walete kwa hiyo hata kama tutavutana haina maana lazima tuwe wapole kwa wazungu ambao ndio wanachangie bajeti zetu kiasi kikubwa kutekeleza miradi ya maendeleo”alisema Mainge

Kuungua kwa soko kuu la mji wa Kibaya kumesababisha hasara ya zaidi ya mil 56 na kwa sasa wafanya biashara wanauzia bidhaa zao juani na wengine kwenye vibada vya kienyeji hali inayowapa usumbufu mkubwa katika kazi hizo

Mwisho      





Maoni