Mwanamke kizimbani kwa madawa ya kulevya Kg 94 Kiteto
NA. MOHAMED HAMAD
Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manayara
limekamata shehena ya madawa ya kulevya aina ya mirungi yenye uzito wa Kg 94
zilizokuwa zikisafirishwa kwenye gari aina ya Noah yenye namba za usajili T 817
TJB
Dereva wa gari hilo na watu waliokuwemo walikimbia na
kulitelekeza gari hilo eneo Jangwani Kijiji cha Bwagamoyo ambapo Polisi
walilichukua na kulihifadhi katika Kituo cha Polisi cha Kiteto kwa uchunguzi
zaidi
Chanzo cha uhakika cha habari hizo kimesema shehema hiyo
inadaiwa kuwa ililengwa kusambazwa Wilayani Kiteto na baadhi ya maeneo ya
Wilaya ya Chemba (Mjirijo) na Kondoa ambako watuhumiwa hao wanadaiwa kuishi
humo
Alisema hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kwa kukutwa na
shehena hiyo ya madawa ya kulenya na kwamba baada ya upelelelezi kukamilika
sheria itafuata mkondo wake kwa wahusika kufikishwa Mahakamani
Kuhusu watuhumiwa kukimbia na kulitelekeza gari hilo
chanzo hicho kilisema ni rahisi kumjua miliki wa gari hilo kupitia Ofisi za TRA
hivyo kama wahusika hawajajitokeza ndani ya siku saba wataenda TRA ili kumjua
mmiliki wa gari hilo
Kwa mujibu wa Sheria imelezwa kuwa mara baada ya
kukamatwa kwa madawa hayo huteketezwa ili yasitumike ndani ya jamii kama
ilivyokusudiwa na mmiliki kwa kusambazwa kwa watu wanaodaiwa kutumia madawa
hayo
Pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa Jeshi la Polisi
kuwakamata wahalifu hao wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya na kufikishwa mahakamani
kila mara watu hao wameendele kuifanya na kusababisha usumbufu mkubwa kwa Jeshi
hilo
Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Akili Mpwapwa
amethibitisha kukamatwa kwa shehena hiyo na kudai kuwa upelelezi unaendelea na
mara baada ya kukamilika na watuhumiwa kukamatwa watafikishwa mahakamani kujibu
tuhuma hizo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni