14
mbaroni kwa tuhuma za mauaji Kiteto
·
Yumo aliyekuwa Diwani wa CCM Namelock
·
10
wako chini ya uangalizi wa Polisi
·
6 bado wanaojiwa na polisi
NA. MOHAMED HAMAD
Jumla ya watu 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Wilayani Kiteto kwa tuhuma za mauaji ya wakulima 10 waliouawa wakiwa
katika makazi yao maeno tofauti Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Awali akisoma mashitaka mbele ya Hakimu Mkazi mahakamani
hapo Mwendesha mashitaka wa Polisi Osca Kusara aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni
Michael Lepunyati ali,Richard Mlahagwa,Kipande Loguto Mgutyo, Lembrisi William,
Daudi Willam, Meshaki Nyoroi Olotipwa, Zacharia Nyoroi Oletipwa
Wengine ni Mosonic Ngangwai, Loserian Isaya,Dijalo
Kalapapai,Paulo Tunyoni Lemonyo (Kibaya )na Mohamed Said Kinyonga wa (Kibaya)
ambapo kwa pamoja wamesomewa mashitaka tisa tofauti ya mauaji
Mwendesha mashtaka huyo wa Polisi alisema washitakiwa hao
wanakabiliwa na kesi mbili tofauti ambapo shitaka la kwanza ni la jumla ya watu
3 waliuawa akiwemo Msagula Madole, Stivin Mashuhulu na mtu mmoa aliyejulikana
kwa jina la Zungu
Na Shitaka la Pili ni la watu sita waliouawa akiwemo
Saidi Hamad ,Emanuel Paulo (Mchungaji wa makanisa ya Pentekoste) mtoto wa
Mchungaji aliyefahamika kwa jina la Shukuru Paulo (12) Mahaule Joseph, Zacharia
Petro, na Rajabu Abdala
Ilielezwa Mahakama hapo kuwa watuhumiwa hao 12 kwa pamoja
walitenda makosa hayo tar 12 mwezi wa
kwanza kuua kinyume na kifungu cha 196 sheria ya makosa ya jinai namba 16 kama
ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
Hata hivyo watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote
mahakamani hapo kwakuwa Mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji
na kwamba kwa mujibu wa mwendesha mashitaka aliomba Hakimu wa Mahakama hiyo
Nestory Barro kutaja tarehe nyingine ili kukamilisha ushahidi
Kwa mujibu wa Hakimu huyo mahakamani hapo alitaka tarehe
nyingine ya kusikiliza kesi hiyo kuwa ni Feb 3 mwaka huu ambapo itawasilishwa
tena na kwamba ushahidi utakapokamilika watyhumiwa hao watapelekwa Mahakama kuu
kwa kesi hiyo kusikilizwa
Hata hivyo baada ya keshi hiyo kuahirishwa mahakamani
hapo MTANZANIA ilizungumza na Shelunde Ngalula Mwanasheria wa Kituo cha Sheria
na Haki za Binadamu (LHRC) ambapo yeye alipongeza jitihada za Jeshi la Polisi
kwa kuweza kuwakamata watuhumiwa na kuwafikisha mahakamani
“Ni kweli kwamba Polisi imefanya kazi yake ya kuwatafuta
watu wanaodaiwa kuwa wauaji wa wenzao hivi karibuni Wilayani Kiteto na
kusababisha vivo vya watu 10 na sisi cha kusimamia ni sheria ifuate mkondo
wake”alisema Mwanasheria huyo
Alisema changamoto iliyopo ni ya kuwa ni jinsi gani ya
kuwabaini wauaji kwani itatakiwa walioua wathibitishiwe bila shaka kuwa
wametenda kosa hilo kwani hakuna anaebisha kuwa hakuna waliouawa na kuongeza
kuwa sheria ifuate Mkoano wake
Hata hivyo miongoni mwa waliouawa ni pamoja na Mchungaji
Emanuel Paulo wa makanisa ya Kipentekoste pamoja na mwanae Shukuru Paulo siku
ya Juma Pili wakati wakienda kanisani hali iliyoibua hisia tofauti za watu
Pia miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na aliyekuwa Diwani
wa kata ya Nameloko LeMichael Lepunyati (CCM) ambaye naye anatuhumiwa katika
mauaji hayo wa watu 10 yaliyotokana na ghasia kati ya wakulima na wafugaji
Wilayahi humo
Kwa Upande wake Kamanda wa Polisi Mkoani Manyara Akili
Mpwapwa alisema kwa sasa juma ya watu 10
wako chini ya uangalizi wa pilisi,saba wameachiwa huru baada ya Polisi
kujiridhisha kuwa hawana hatia na sita bado wanahojiwa
Wakati jitihada hizi zinaendelea baadhi ya wananchi
Wilayani Kiteto wamethibitisha kuwa hali ni shwari kutokana na kufikishwa
mahakamani watuhumiwa hao na kuongeza kuwa ili kukomesha vitendo hivi sheria
ifuate mkondi wake bila kumwonea mtu
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni