Polisi
Kiteto wakanusha uporaji wa simu.
·
Waeleza wanaopora watu simu,pesa
·
Wasema mbali na uporaji pia watu wanapigwa
NA. MOHAMED HAMAD.
Jeshi la Polisi Wilayani Kiteto Mkoani Manyara
limekanusha kuwa hakuna Askari aliyehusika kupora simu,pesa na baadhi ya mali
za watu wanaotakiwa kuondoka eneo la
Emboley Murtangos kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari Nchini
Akizungumza hayo Foka Dinya Mkuu wa Polisi Wilayani
Kiteto leo (jana) amesema siku waliyoporwa watu simu Polisi hawakwenda kwenye
operesheni hiyo na waliokuwa wameenda ni Askari Migambo ambao huambatana nao
kwenye Operesheni hiyo
“Tena aliyeandika habari hii nataka kumfahamu amepata
wapi habari hizi,ninachojua siku hiyo pamoja na kwamba Polisi tunahusika kwenda
kwenye Operesheni hiyo hatukuwepo siku hiyo Migambo ndio walienda”alisema
Dinya
Wakieleza juu ya Operesheni hiyo mmoja wa maaskari ambaye
jina lake limehifadhiwa alisema ktukana na sakata hilo walibaini mmoja wa
Askari Migambo ambaye alihusika na kwamba ghatua za kinidhamu zinachukuliwa
Akizungumzia sakata hilo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Umbulla
alisema hana taarifa za watu hao kuporwa simu na mali zao na kuongeza kama
kweli lipo tatizo la namna hiyo Jeshi la Polisi litashughulikia
“Askari tumewapa masharti kuwa wasichukue kitu chochote
cha mtuhumiwa hadi watakapowakabidhi Polisi na kama kuna aliyepora sheria kali
dhidi yake zitafuata kwa kila atakaye husika”alisema Umbulla
Mkuu huyo wa Wilaya alieleza kuwa kuna mambo mawili
yanayochanganywa na wananchi kuwa lipo agizo la Waziri Mkuu kutaka waliofanya
mauaji ya watu kumi wakamatwe na pia kwa Wilaya tuna operesheni maalumu ya
kuwatoa wavamizi katika eneo la Emboley Murtangos
Kwa mujibu Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Bruno
Bongole ameliambia MTANZANIA kuwa jumla ya watu 99 wamekamatwa kwa tuhuma za
kukutwa ndani ya eneo hilo huku 66 wakiwa wamefunguliwa mashitaka na 33
wakisubiri kuingizwa mahakamani kusomewa mashitaka yao
Baadhi ya wadadisi wa mambo wamesema kukamatwa kwa watu
hao kumetokana na wengi wao kutojua mipaka ya eneo hilo utokana na madai kuwa
kuna mkanganyiko wa mipaka uliofanya na Halamshauri baada ya kumalizika Kesi ta
Msingi
Baadhi ya wananchi waliopo katika vijiji vinavyodaiwa
kuunda hifadhi hiyo wamesema awali walikubaliana kutenga eneo hilo, baada ya
kesi kumalizika eneo hilo limemega maeneo ya kilimo hivyo kusababisha
malalamiko ambayo hadi sasa haijulikani mwafaka wake huku watu wakiendelea
kukamatwa na kufikishwa mahakamani
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni