SERIKALI KITETO YAZIDI KUKAIDI AGIZO LA PINDA

SERIKALI YA KITETO YAKAIDI AGIZO LA PINDA

Ninachoamini katika maisha ya binadamu ni kwamba kila mtu huwa na uelewa wake , na uelewa huwa unazidiana sasa kwakuanzia hapa nianza makala yangu hii kwa kuchambua baadhi ya mambo aliyokuwa amesyasema Wairi Mkuu Pinda alipozungumza na wananchi tar 16.1.2014

Waziri Pinda alifika Kiteto kwaajili ya kutoa pole kwa ndugu na jamaa ya waliopoteza ndugu zao baada ya kuuuawa na watu ambao walijifanya kuwa wanauchungu wa kulinza mazingira kuliko wengine kwa kuwapiga risai na kuwakata kata mapanga

Kitendo hicho hakikuifurahisha Serikali ambapo Waziri Mkuu Pinda alilazimika kufika Wilayani Kiteto ili kutoa tamko la Serikali pamoja na kuagiza Jeshi la Polisi kuwakamata wahusika mara moja kisha kuwafikisha mahakamani ili sheria ifuate mkondo wake

Wakati hayo yanatakiwa kuwa kama yalivyo Waziri Mkuu aliwataka wananchi kutii sheria bila shuruti kwa kuwataka waondoke kwenye eneo la Emboley Murtangos ambalo alidai kuwa ni hifadhi ya Vijiji saba kwaajilinya matumizi ya baadaye

Hata hivyo Pinda hakusita kuonyesha alivyochukizwa na kazi iliyofanya na kikundi hicho cha mauaji akisema kilichoma nyumba zikiwa nan chakula na kuitaka Serikali kuwapatia chakula wahanga hao jambo ambalo toka atoe ahadi Jan 16 hadi leo hakuweza kuhakikisha wananchi hao wanapata huduma

Pia kabla ta kuondolewa kwa nguvu viongozi hao walitakiwa ktoa elimu ili wananchi waliopo watoke bila shuruti akifafanua kuwa atakaye weza kutatua migogoro na kuishi kwa amani atakuwa mbora hadi kwa mungu


Pia katika zoezi hili imedaiwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshaur ya Wilaya Jane Mutagurwa anazidi kukaidi agizo la Waziri Mkuu  kwa kuanza operesheni ya kwatoa wakulima katika maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa imeamriwa

Mwisho


Maoni