VIGOGO WA CCM WAMIMINIKA KITETO KUNUSURU CHAMA

Vigogo wa  CCM wamiminika Kiteto kunusuru chama
  • Wapo wabung,Manaibu Waziri 
Na Mohamed Hamad
Katika hali isiyokuwa ya kawaida upepo mbaya unazidi kuvuma kwenye ngome ya Chama cha Mapinduzi CCM baada ya mikutano yao kuonekana kuwa na watu wachache kunadi wagombea wao katika kata mbili za marudio Wilayani Kiteto

Kata hizo ni Partimbo na Loolera ambako madiwai wake walifariki katika mazingira ya kutatanisha na kusababisha kata hiyo kukosa wawakilishi ambapo sasa uchaguzi mdogo umeitishwa kupata viongozi wa kuongoza kata hizo

Aliyekuwa Diwani wa kata ya Partimbo ni Julias Ole Nairinga ambaye alifariki baada ya kuanguka ghafta akiwa nyumbani kwake na Kone Lembile Diwani wa Loolera  ambaye naye alifariki baada ya kuanguka akiwa anachunga mifugo yake

Hata hivyo baadhi ya wadadisi wa mambo ya kisiasa walisema ugumu huo unatokana na maeneo hayo kuwa na migogoro ya ardhi iliyosababisa zaidi ya watu 16 kupoteza maisha huku 54 wakiwa wamejerihiwa kwa kupigwa wakiwa mashambani

Maoni