KCS
Forum yaibua ufisadi mpya Kiteto
- Madiwani wadai wanapotezwa na kiingereza
- Wadau wazitaka mamlaka kuingilia kati kunusuru Halm
Na. Mohamed Hamad
MTANDAO wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Wilayani
Kiteto (KCS Forum) Kiteto Civil Society) umeibua ufisadi Halamashauri ya Wilaya
ya Kiteto hali iliyosababisha manung’uniko ya wananchi kwa kutokamilika miradi
ya maendeleo pamoja na kupata hati chafu kila mara
Taarifa iliyowasilishwa kwenye kikao cha wadau wa
maendeleo Wilayani humo imebaini kuwepo mikataba feki inayofungwa na
Halamshauri na kuruhusu mianya ya ulaji dhidi watendaji pamoja na kutolewa tenda
kirafiki na kusababisha kutopatikana kwa uduma zinazostahili
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa njia ya (power Pointer)
Abdul Msonde na Lilian John wajumbe wa timu ya ufuatiliaji uwajibikaji umma SAM
walisema fedha zinazotolewa na Serikali hazilingani na thamani halisi ya miradi
iliyopo vijijini
Pia taarifa zinazoandaliwa kwa kiswahili na kiingereza kwa
walengwa zinatofautiana tarakimu za fedha jambo ambalo uwazi na ukweli unakosekana
kwa watumishi wanaoandaa taarifa hizo dhidi ya wananchi hao
“Taarifa ya utekelezaji robo ya nne ya mwaka 2010//2011 inaonyesha
fedha kutoka BFFS kutekeleza miradi ya maendeleo zilikuwa ni mil 342,850,000
ambapo taafifa hiyo hiyo kwa kiswahili inaonyesha mil 445,700,000 ambazo zilipangwa
kwa uchimbaji visima 15 vya maji,
Tofauti na Taarifa ya kiingereza inayoonyesha kuwa fedha
zilipagwa kwaajili ya upimaji na usanifu wa maji vijiji 12 kazi ambayo taarifa
hiyo imesema haionyeshi kazi iliyofanyika” alisema Msonde
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa za mdhibiti na mkaguzi
mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) 2011/2012 imeeleza kuwa kuna hoja za ukaguzi
zenye jumla ya mil 526,179,669 ambazo Mkurugenzi alitakiwa kutafuta nyaraka
zilizokosekana bila mafanikio
Pia taarifa hiyo ya CAG imeeleza kuwa kuna malipo yenye
nyaraka pungufu mil 7,211,499.99, manunuzi ya shajala ambayo hayajathibitishwa
mil 22,832,083, kiasi cha mil 513,613,560 zilizokusanywa na mawakala
kutopelekwa Benki hazikuonekana
Kwa upande wake Lilian John akiwasilisha taarifa ya hali
halisi ya miradi iliyopo mjini na vijijini alisema kuwa miradi mingi iliyotumia
fedha nyingi za wananchi imetelekezwa baada ya kutokamilika kwake huku
kukikosekana jitihada za kuiboresha
“Kuna Tanki la maji lenye thamani ya zaidi ya mil 200
lililolenga kuondoa adha ya maji mjini Kibaya ambalo liziduliwe na aliyekuwa
makamu wa Rais Alli Mohamed Shein mwaka 2009 hadi leo maji hayakuweza kuingia
kama ilivyokusudiwa”alisema Lilian
Alisema mbali na mradi huo pia kuna miradi mingi ya
majosho, pamoja na maji kwaajili ya Binadamu na mifugo imetelekezwa kwa
kujengwa chini ya kiwango huku viongozi wakiwa kimya bila kutafuta ufumbuzi wa
wananchi kunufaika na miradi hiyo
Kwa upande wake Hassan Benzi Diwani (CCM) alisema tatizo
lililopo ni kuwepo kwa madiwani ni kuwepo kwa taarifa zinazo andaliwa kwa lugha
ya Kiiingereza ambayo sio rafiki kwa madiwani hivyo kujikuta wakipitisha
masuala mengi bila wao kujua
Akichangia taarifa hiyo Hassani Konki (mwananchi) alisema
hakuna sababu ya kuwa watumishi wasiokuwa waadilifu ndani ya Halamshauri
akisema badala ya Serikali kusubiri madhara waondoke na wachukuliwe hatua juu
ya ubadhirifu
“Kiteto hatuna nafasi ya kuendelea kuwa na wezi,watumishi
wana nawiri,wanatakata,wanajijenga kumbe wanatuhujumu, kama kuna taarifa ya CAG
inasema kuna wizi kiasi hicho muda wote wanasubiri nini kuchukua hatua”?
Naye Mashaka Saidi Fundi mwangalizi wa haki za Binadamu
alisema Serikali isisubiri mwananchi ambaye kwanza uelewa wake ni mdogo achukue
hatua na kuongeza kuwa anataka kuona viongozi wa Halamshauri ya Wilaya ya
Kiteto wanawajibika katika nafasi zao la sivyo ataenda mahakamani kumshitaki
Mkurugenzi
Bakari Maunganya (mwananchi) alisema kinachosababisa
kuwepo kwa matatizo ni Viongozi kulindana, akitolea mfano wa jinsi matatiozo
yanavyowakumba wananchi wa kiteto kuwa kila mara wananchi wanalalamika bila
hatua kuchukuliwa
Kwa upande wake Mainge Lemalali Mwenyekiti wa Halamshauri
ya Wilaya ya Kiteto kuhusu kutokamilika kwa miradi hiyo alisema ni kutokana na
wanachi kushindwa kuchangia asilimia 20% katika miradi hiyo
Kuhusu hoja za ukaguzi Lemalali alisema zipo jitihada
zilizofanywa na Serikali kwa watumishi wake akisema walio onekana kuwa na
matatizo yaliyozidi kiwango wamehamishwa na wengine hawatavumilika
watachukuliwa hatua
Alisema Wilaya ya Kiteto sio ya majaribio tena kwani
madhara makubwa yamejitokeza kwenye miradi ya wananchi na kuongeza kuna watumishi
wengi wamehamishwa na wataendelea kuhamishwa kwa kutowajibika kwao
Akieleza malengo ya kikao hicho Yusuph Mohamed Mtatibu wa
KCS Forum alisema ni kutoa mrejesho wa taarifa ya ufuatiliaji utelelezaji wa
miradi ya maji, kilimo, na mifugo iliyotekelezwa toka mwaka 2010 hadi 2012 kazi
ambayo ilifadhiliwa na Ubalozi wa Switzeland
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni