CCM
Kiteto wamchachamalia Mbunge
·
Wamtaka ajitokeze kukemea mauaji
NA.MOHAMED HAMAD
KATIBU wa Itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM
Wilayani Kiteto Chrispipher Ole Parmet ameibuka na kumtaka Mbunge wa Jimbo la
Kiteto Benedict Ole Nangoro kujitokeza na kukemea mauaji yanayoendelea
kujitokeza Wilayani humo
Parmet amesema hayo siku ya wazazi kata ya Chapakazi alidai
ukimya wa Mbunge Nangoro unawapa shaka wananchi na hasa wanachama wa chama
chake cha CCM ambao walitumia muda mwingi
kumpata kiongozi hayo
"Tunataka mbunge wetu ajitokeze hadharani akemea
maovu yanayoendelea hasa mauaji ambayo yanazidi kuwagawa wananchi kwa itikadi
za ukabila na hata vyama hali inayosababisha wengi wao kukosa imani na Serikali
yao”alisema Parmet
Migogoro ya ardhi Mkoani Manyara hasa Kiteto imekithiri
kutokana na baadhi ya Viogozi kutokuwa waadilifu na kujali maslahi binafsi
ambapo kwa muda mrefu imeendelea kurindika huku Viongozi wakionekana kutokuwa
na dhamira ya dhati kumaliza
Kwa kipindi cha miezi minne zaidi ya wananchi 16
wamepoteza maisha huku zaidi ya 50 wakijeruhiwa kutokana na migogoro hiyo huku
Viongozi wa Wilaya wakikwepa kuongea na wakulima na wafugaji kuwataka waachane
na mgogoro huo
Parmeti amesema katika hali isiyokuwa ya kawaida Mbunge
wao Benedict Nangoro (CCM) ameendelea kuwa kimya asijitokeze kukemea mauaji ayo
hali inayotafsiriwa tofauti na kusababisha watu kuwa na chuki dhidi yake
“Chama tumemtaka Mwenyekiti kuonana na Mbunge ana kwa ana
kuelezwa ajitokeze kwa wapiga kura wake na hata kwenda kuwapa pole wahanga wa
mauaji hayo pamoja na kutoa msimamo wake kuhusiana na eneo hilo
linalogombaniwa”
Alisema Migogoro ya ardhi Wilayani Kiteto inasababishwa
na baadhi ya viongozi Wilayani humo ambao wana maslahi na eneo la Emboley
Murtangos kutaka kutimiza matakwa ya jamii moja ya kifugaji ili waweze
kunufaika na eneo hilo
Akifafanua zaidi Katibu huyo amesema eneo la Emboley
Murtangos lina utata mkubwa ambalo hata Waziri Mkuu wa Mizengo Pinda baada ya
mauaji aliagiza kutazamwa upya juu ya eneo hilo ambalo linaonekana kuwepo kwa
utata wa uanzishwaji wake
Alisema baada ya kutembelea eneo hilo alichokiona sio
hifadhi kama inavyodaiwa na Viongozi wa Wilaya bali alikuwa mashamba ya
wakulima na kusisitiza viongozi wa Halmashauri
kuangalia lengo la uanzishwaji wa hifadhi hiyo upya pamoja na mipaka
yake
Pia Waziri Mkuu alishangazwa kusikia jamii ya kifugaji
wamasai wamechangishwa fedha za kuwatoa wakulima katika eneo hilo la Emboley
Murtangos hali aliyodaiwa kuleta uvunjifu wa amani na kusababisha kikundi cha
watu kuibuka na kufanya mauaji katika maeneo hayo
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni