KATUBU WA UCHUMI CCM KITETO AMCHANA MB.NANGORO

Katika hali ya kuonyesha kuwa wananchi wanakerwa na utendaji kazi wa baadhi ya viongozi wa Serikali na hata Siasa Christopher Ole Parmet Katibu wa Uchumi wa Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Kiteto ameibuka akisema Benedicti Ole Nangoro Mbunge wa Jimbo la Kiteto amekuwa kiongozi wa Pekee ambaye ameshindwa kuwa na utu kwa wananchi wake

Akizungumza hayo kwenye sherehe za siku ya Wazazi za Chama cha Mapinduzi CCM Wilayani humo Parmeti amesema kitendo cha Mbunge wao kushindwa kukemea mauaji yanayoendelea kujitokeza ni aibu na hakipaswi kuigwa na kiongozi yoyote hapa nchini

Amesema toka mauaji yaanze kujitokeza na kufikia zaidi ya watu 16 huku wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa Mbunge Nangoro ameshindwa hata kutoa pole kwa wananchi wake hali inayotafsiriwa tofauti na makundi mbalimbali ndani ya jamii ya wanakiteto

"Namwomba Mbunge wetu ajitokeze hadharani akemee mauaji yanayoendelea kujitokeza kila kukicha ukimya wake unatupa shaka sisi wananchi na hata viongozi wenzake ambao tuko naye kwani hatuna majibu juu ya kinachojitokeza "alisema Parmeti huku akipigiwa makofi

Sherehe za siku ya wazazi Kiwilaya zimefanyika kata ya chapakazi ambapo mgeni rasmi alikuwa Rajabu Kinyua Mwenyekiti wa CCM Wilaya ambapo aliwataka wananchi kufanya maamuzi magumu dhidi ya viongozi wao ambayo kwa sasa wanaonekana kuwasaliti.

Maoni