MKULIMA MWINGINE AUAWA KWA KUCHINJWA KITETO

Mkulima Kiteto auawa kwa kuchinjwa
*       Kamati ya usalama yaketi kwa dharura
*       CCM yalaani yatoa tamko

NA. MOHAMED HAMAD

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Masudi mkulima (mgogo) mkazi
wa kitongoji cha Orkeri Wilayani Kiteto Mkoani Manyara, ameuawa kwa
kukatwa kwa kitu chenye ncha kali shingoni (kuchinjwa) na watu
wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji wanaovamia makazi ya wakulima

Tukio hilo limetokea April 3 mwaka huu baada ya baadhi ya jamii ya
kifugaji (wamasai) kuvamia wakulima kwa kuwapiga kisha kuwachomea
makazi yao ili waweze kuondoka na kuyaacha maeneo yao ambayo
yatatumika kwa shughuli za ufugaji

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara ambae pia ni Kamishna mwandamizi
wa wa  Polisi (SACP) Deusdedit Nsimeki ameliambia MTANZANIA kuwa
matukio ya mauaji Kiteto yamekuwa yakijitokeza kutokana na jamii za
wakulima na wafugaji kugombea ardhi

"Huwezi kuamini mwandishi suala hili linaonekana kuwa na mvuto mkubwa
Wilayani hapa kwani baadhi ya Viongozi wa ngazi mbalimbali wakiwemo
wana Siasa wanadaiwa  kunufaika na migogoro hiyo kwa namna moja ama
nyingine"

"Jeshi la Polisi tumejipanga  hatutamwonea mtu, sheria itafuata mkondo
wake awe mwanasiasa au kiongozi yotote wa Serikali atakaye husika
tutamkamata na kumfikisha mahakamani ili sheria ifuate  mkondo
wake"alisema Kamanda Nsimeki

Alisema wapo wanasiasa ambao kwa namna moja ama nyingine wameonekana
kujitokeza katika mgogoro huu, wakiwemo baadhi ya viongozi wa
Halamshauri na kusababisha mgogoro kuendelea

Kamanda Nsimeki alisema hakuna mtu anayeshikiliwa kwa mauaji hayo na
kwamba Jeshi la Polisi kiteto likiongozwa na Mkuu wa Polisi Mrakibu
Mwandamizi Evaristi Chuwa watahakikisha waliohusika na mauaji hayo
wanakamatwa na kufikishwa mahakamani

Kutokana na tukio hilo kamati ya Ulinzin na usalama imeketi katika
kikao cha dharura mbapo pamoja na mambo mengine imelaani mauaji hayo
na kusema jitihada zitafanyi kakabiliana na mauaji hayo

KAMATI YA SIASA
Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Kiteto kimelaani mauaji ya kinyama
yaliyofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuwa wanatokana na jamii
ya kifugaji wamasai na kuiagiza Serikali kutokomeza vitendo vya mauaji
vinavyojitokeza kila mara

Akizungumza hayo Abeid Maila mara baada ya kwenda kushuhudia mwili wa
marehemu uliopo katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto alisema, huo ni
uhalifu ambao Serikali ya Chama cha Mapinduzi CCM haiwezi kuvumilia

Maila ameitaka kamati ya Ulinzi na usalama Kiteto kuhakikisha
inavikomesha vitendo vya mauaji ya mara kwa mara vinavyoendelea
kujitokeza na kusababisha wananchi kukosa imani na Serikali yao ambayo
kqwa sasa nndio iko madarakani

"Sisi Chama tumechukizwa na kitendo hiki tumekutana kamati ya siasa
kushuhudia mwili wa ndugu yetu ambaye amekatishwa maisha yake kwa
maksudi, na vitendo hivi vinatisha sana iko haja kwa Serikakali
tunayoiongoza kufanya kazihii kwa makini natupate taarifa"

 "Waziri Mkuu Miizengo Pinda alipofika hapa alituliza munkari wa
wananchi kwa kuiagiza Serikali kufanya mambo mbalimbali yakiwemo
kutenga maeneo ya kilimo na mifugo lakini toka aondoke kazi hiyo
haijafanyika"

Kwa mujibu wa Katibu huyo wa CCM alisema Waziri Mkuu pamoja na mambo
mengine baada ya kuwasili Kiteto kutokana na mauaji ya zaidi ya watu
16 mapemamwakahuu aliitaka Serikakli ya Kiteto kuhakikisha amani
inarejeshwa kwa kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji

Pia alisema ili kuondoa tofauti ya mkulima na mfugaji maeneo ya kilimo
na mifugo yawekewe mipaka ambayo itasaidia pande hizo kutoingiliana
kwa shughuli za kiuchumi ambazo zinafanywa na wenyeji hao

WANANCHI
Baadhi ya wananchi wamesema kifo cha mkulima huyo ni mwendelezo wa
mauaji yanayofanywa na watu wa jamii ya kifugaji baadhi ya wamasai
ambao inadaiwa chanzo ni Halmshauri ya Wilaya kuwagawa wananchi kwa
itikadi ya kikabila

Akizungumza hayo  Luka Ngidi (30) majeruhi aliyelazwa kwa kujeruhiwa
na wafugaji akiiwa shambani kwake baada ya kutembelewa na kamati hiyo
ya siasa ya Wilaya amesema Serikali ya Kiteto iko likizo na ndio maana
kila kukicha mauaji hayaishi huku viongozi wakibakia kushiriki mazishi

" Naweza kusema mimi nilikwisha kufa tu, maana nilizingirwa na wamasai
shambani kwangu baada ya ngombe kuingizwa kwa nguvu, nilipigwa fimbo
nyingi sana nawashukurui madaktari sana wameokoa maisha yangu"

Serikali hii iko likizo hapa hatuna Mbunge wala Mkuu wa Wilaya
tunaishi kama hatuna Serikali nawaomba kwakuwa ninyi ndio mmeweka hii
Serikali madarakani wasimamieni hawa viongozi tukifa wataongoza akina
nani alisenma kwa machungu majeruhi huyo

Kwa upande wake Dkt Thomas Ndalio akieleza hakli ya mgonjwa huyo
alisema kwa sasa a
naendelea vizuri baada ya kupata matibabu, akisisitiza kuwa hali yake
ilikuwa mbaya na sasa anaweza hata kuongea vizuri na hata kula

Kuhusu marehemu huyo alisema amekatwa nma kitu chene ncha kali
shingoni kasha kuchomwa na mkuki hali iliyompelekea kifo hicho ambacho
kimevuta hisia za watu wengi wilayani kiteto akisisitiza kuwa mauaji
hayo yataisha endapo Serikali iitaamua kukabiliana nayo ipasavyo

mwisho

Maoni