DC Kiteto
mipaka ni tatizo la mauaji ya wakulima,wafugaji
NA. MOHAMED HAMAD
Mauaji yanayoendelea kujitokeza Wilayani
Kiteto Mkoani Manyara kati ya walikuma na wafugaji inasababishwa na
kutobainishwa kwa mipaka kwa muda mrefu hivyo kila mtu kufanya atakavyo
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya ya
Kiteto Martha Jaki Umbulla kwenye mkutano mkuu wa Kijiji cha Kimana
uliohudhuriwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama pamoja na baadhi ya
viongozi waandamizi wa Mkoa wa manyara
“Tatizo tulilonalo hapa ni wananchi
kushindwa kutambua wako eneo gani katika kufanya shughuli zao za kilimo ama
ufugaji kwani awali tulitenga maeneo hayo kwa utaratibu maalimu na baadae
ukavurugika”alisema Umbulla
Kinachoniudhi sana ni kuona idadi kubwa ya
watu kutoka maeneo ya jirani kuja kuhodhi maeneo makubwa ya adhi huku Kiteto
kwa shuhuli za kilimo huku wanaKiteto wakiwa hawana hata hatua moja ya kulima
Amesema utaratibu huu haukubaliki na hata
kama walipewa na Serikali za vijiji kwa kuhonga kwao haikubaliki lazima wanyan’ganywe
tuanze upya utaratibu huu wa kugawa ardhi kulingana na idadi ya wananchi wetu
tulionao
“Unamkuta mtu ana zaidi ya ekari elfu 3
huko porini na hata kuingilika inakuwa shida huu sio utaratibu wa matumizi bora
ya ardhi na hata hiyo Halamshauri haiwezi kunufaika na chochote humo kwani hata
usalama wenyewe kufika ni mdogo”
Kuhusu eneo hilo kuitwa hifadhi ya Emboley
Murtangos Umbulla alisema vijiji saba vilikwisha tenga eneo miaka ya 2000 kwa
makubalian maalumu na vikao vya kisheria pamoja na kumbwa kuna wajanja wachache
waliiba mihutasari bado tunatambua eneo hilo
Kauli hiyo iliibia hoja nyingi kwa wananchi
hao wakisema kamwe hawakubalinani na jina hilo la Emboley Murtangoso bali
wanatambua kutenga hifadhi kwakuwa wanachofahamu kila kijiji kilitenga eneo
lake la matumizi ya baadaye na sio kama inavyoelezwa
“Tusipotoshane hapa baada ya kuharibika
jambo hili, ninachokubuka mimi ni mwanzilishi wa mipango hii mwaka 2000
tulikuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi ambapo hapo tulisema tuwe na
sehemu ya akiba kidogo kwa watu watakao ongezeka wapatiwa”alisema Bakari
Maunganya
Alisema wakati wanatenga hakukuwa na kitu
kinachoitwa Emboley Murtangos kama eneo linavyolazimishwa kutambulika kisheria
kwa nguvu ya wachache ya upande mmoja (wafugaji) kulitumia kwa makazi yao
pamoja na kulisha mifugo …(makofi)
Kwa upande wake Wilson Ngolanya (mkulima wa
kimana) alisema baada ya kutenga eneo hilo jamii ya kifugaji (wamasai)
walionekana kuhodhi eneo hilo kwa shughuli zao hali iliyosababisha wakulima nao
kuingia na kuanza shughuli za kilimo
Katika mvutano huo Ngolanya alisema hapo
ndipo chanzo cha mauaji yakaanza kwa jamii ya baadhi ya kifugaji kuwa na
mamlaka ya kuanza kufanya watakavyo kama kuvamia wakulima na kuwaua huku
Serikali ikiendelea kuwaunga mkono kwa kuwakamata wakulima na kuwafunga
Nae Anon Chui (mkulima) alisema adui namba
moja wa matatizo hayo ni Serikali yao kuanzia ngazi ya kijiji,kata,Wilaya na
hata Taifa hasa pale ilipoungana na wafugaji kuwachangisha fedha kisha
kuwaondoa wakulima katika maeneo hayo
Amesema kama wakulima na wafugaji
wanakamatwa kwa kuitwa wachochezi na kufikishwa mahakamani hali kadhalika viongozi hao nao wanatakiwa
kukamatwa kwa kuanzisha mipango mibovu na kuiunga mkono
Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya alisema
Serikali imejipanga kuainisha mipaka ili kila kundi liweze kutambua eneo lake wakati
wanafanya shughuli zao za kujipatia kipato akisisitiza kuwa eneo hilo
lilitengwa na vijiji saba na mahakama ikaamuru pasiwepo na shuguli za ibinadamu
huko
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni