Madiwani
13 Kiteto kuhojiwa kuhusu Hifadhi ya Emboley
NA.MOHAMED HAMAD
JUMLA ya madiwani 13 wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto
Mkoani Manyara wanatarajia kukutana na tume maalumu ya makamishna waliopo
Mkoani Manyara juu ya sakata la migogoro ya ardhi Wilayani humo inayoendelea
kusababisha maafa
Madiwani hao wamepata Barua kutoka ofisi ya mkuu wa
Wilaya ya Kiteto kwa njia ya dispachi kwa lengo la kuonyesha umuhimu ambao unakusudiwa
kuleta matunda ya kuunganisha wakulima na wafugaji waliopoteza mahasimiana na na
kusababisha mauaji ya mara kwa mara
“Napata shaka sana kwenda kuhojiwa na makamishna hao sijajua
nini wanataka kwangu hasa kuhusiana na migogoro ya ardhi kwani mbona kila kitu
kinajulikana na awali walichukua vielelezo vingi tu na nyaraka?”alisema Diwani
mmoja Wilayani humo
Alisema Serikali ikitaka kukomesha mauaji Kiteto inaweza
lakini kama itaingiza siasa kwa kulindana hasa uchama,ukabila,urafiki watu
watazidi kupoteza maisha huku wengi wao wakiwa maskini kukatishwa maisha yao
bila sababu
Kidawa Othmani Kidawa Diwani wa Kata ya Matui ni miongoni
mwa madiwani waliopata barua ya wito rasmi ambapo pamoja na mambo mengine
amesema jambo hili ni zito linahitahi umahiri na umakini katika kulishuhulikia
kitokana na kushamiri siasa, ukabila na rushwa
Uchunguzi uliofanywa na MTANZANIA umebaini kuwa zaidi ya
makundi manee yanaendelea kuhojiwa kutokana na sakata la migogoro ya ardhi
Kiteto wakiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Jaki Umbulal,aliyekuwa
Mkurugenzi Jane Mutagurwa ambaye sasa amehama
Wengine ni Mbunge wa Jimbo la Kiteto Benedicti Ole
Nangoro,Mwenyekiti wa Halmashauri Mainge Lemalali,Afisa habari wa Halmashauri
Maiko William,pamoja na maafisaa wengine ambao majina yao hayajafahamika mapema
Mbali na viongozi hao pia kada ya wanasiasa (madiwani) 13
wamepatiwa barua rasmi kwaajili ya kwenda kuhojiwa kuhusu sakata hilo ambalo
linazidi kuchukuwa sura mpya kila kukicha kwa wakulima kupoteza maisha pamoja
na majerhi mara kwa mara na kundi la wafugaji
Hata hivyo habari za uhakika zinaeleza kuwa wenyeviti wa
vijiji saba pamoja na watendaji wao katika vijiji saba vilivyounda eneo hilo la
hifadhi ya Emboley nao wanaendelea kuhojiwa kuhusu uhalali wa hifadhi hiyo na
kama ilifuata taratibu za uanzishwaji
Wakati mahojiano haya yakiendelea jamii ya kifugaji
wamasai wamezidi kuwajeruhi wakulima wakiwa mashambani pamoja na kulisha mifugo
yao hali iliyodaiwa kuwa inazidi kuleta chuki uhasama pamoja na wananchi kukosa
imani na Serikali yao
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni