Kinana
awashukia viongozi wa Serikali
- ·
Asema wanachangia migogoro ya ardhi
- ·
Aapa kuwasilisha kilio cha wananchi kwa Rais
- ·
Akiri migogoro yaanzia kwenye CCM
NA.MOHAMED HAMAD
KATIBU Mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Abrahamani
Kinana amewashukia viongozi wa Serikali kushindwa kuwahudumia wananchi hali inayo
sababisha wakose imani na Serikali yao
Akizungumza kwenye ziara yake Wilayani Mkoani Manyara
Kinana amesema kila kona ya nchi kuna migogoro ya ardhi na kuahidi kilio hicho
kuwasilifikisha kwa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ili aweze kutafutia
ufumbuzi
Alisema migogoro ya adhi imekuwa tishio kwa wananchi
kuuwana wenyewe kwa kusababishiwa na baadhi ya viongozi wasiokuwa waadilifu
ambao wamekuwa wakiitumia migogoro hiyo kama vyanzo vya mapato yao
“Migogoro hii inaanzia ndani ya chama changu cha CCM, siamini
kama kuna jitihada za vongozi wa Serikali zilizofanyika kutatua migogoro
naahidi suala hili nitaenda kumweleza Mhe Rais ili aweze kuishuhulikia”
Wakati mwingine viongozi hatuonyeshi dhamira ya dhati
kushuhulikia matatizo,tunaenda kwa wananchi usikiliza migogoro na kurejea
tukiwa hatujaishihulikia,lakizima madhara yajitokeze alisema Kinana huku
wananchi wakipiga makofi mengi
Alisema suala hili mwenye uwezo kulishuhulikia ni Mhe Rai
Peke yake na ndio maana hakutaka kusikiliza kauli za wananchi kwenye baada ya kusomewa taarifa nyingi za chama na
hata Serikali
Kuhusu suala la katiba mpya,Katibu mkuu huyo wa CCM
alisema wananchi wa Tanzania hawaihitaji bali hilo ni shinikizo la baadhi ya
viongozi wakitaka kuingia madarakan kwa kushinikiza umma kutaka katiba
“Wananchi wanahitaji huduma za jamii kama vile maji,
afya, barabara na shule na sio katiba kwani ziko nchi zinazoongozwa bila katiba
mfano Uingereza mbona wananchi wanaishi kama haja ni kuwa na katiba”alihoji
Kinana
Baadhi ya wananchi wa Kibaya katika mkutano huo walikosoa
hutuba hiyo wakisema walichotarajia ni kusikia hatua zaidi kuhusu migogoro ya
ardhi ambayo imesababisha zaidi ya watu 16 kufunguliwa kesi za mauaji huku 77
wakifungwa na wengine zaidi ya kumi kupoteza maisha kwa kuuawa
“Nilitegemea Kinana asema viongozi waliohusika
kusababisha vurugu hizo wamechukuliwa hatua hii,na sio kuja na kusema naenda
kwa Rais, hiyo haitoshi kwani Rais anajua kila kitu tunataka kuona hatua
zikichukuliwa”alisema Mashaka Saidi Fundi mwananchi wa Kibaya
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni