Silaha za moto  zatumika kulisha mashamba ya wakulima Kiteto

NA.MOHAMED HAMAD
BAADHI ya wafugaji (wamasai) wilayani Kiteto mkoani Manyara wameanza kutumia silaha kali za moto kutishia wakulima  mashambani wakimbie ili wachunge mifugo yao kwenye mashamba kama njia ya kuwakomoa waondoke katika maeneo hayo

Wakizungumza na MTANZANIA wananchi wa vijiji vya mbeli, Lerug, olpopong,mbigili na kimana wamesema kitendo cha mifugo kuingiza mifugo shambani ni cha kinyama ambapo wameomba Serikali kuingilia kati

Wamesema awali Serikali ilitoa agizo kwa Halamshauri ya Wilaya  kubainisha mipaka ya maeneo ya wakulima na wafugaji toka mwanzo mwa mwaka huu 2014 bila mafanikio

“Waziri Mkuu alipofika hapa mwezi wa pili kushuhudia mauaji ya zaidi ya watu kumi waliouawa mashambani aliagiza kutengwe maeneo kati ya wakulima na wafugaji ili tusiingiliane”alisema mmoja wa wakulima

Alisema toka agizo hilo litolew na hadi leo hakuna kilichofanyika na badala yake kila kukicha kumekuwepo na uhasama kati ya wakulima na wafugaji ambapo sasa wameamua kutumia bunduki kutisha wakulima ili wachunge

Akizungumza kwa masikitiko Charles Mgatha mmoja wa viongozi wa dini ambaye pia ni mkulima anasema hali sio shwari Wilayani humo baada ya Jeshi la Polisi kushindwa kutoa ushirikiano kukabiliana na wafugaji


“Mkulima anapoenda kutoa taarifa za kulishiwa mazao yake cha kwanza anaulizwa unamafuta ya kuweka kwenye gari? Lakini pia anaulizwa kama yupo kwenye hifadhi, hifadhi gani wanayojua polisi wakati Serikali ilikwisha kutoa maelekezo juu ya maeneo yenye mgogoro” alihoji mgatha

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Jaki Umbula aliwataka Halmashauri kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji kama alivyoagiza Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ziara yake Wilayani humo hivi karibuni

Kutokana na sakata hilo hufu ya kuibuka tena mgogoro kati ya wakulima na wafugaji imeanza kujitokeza kutokana na jamii iyo ya kifugaji kuchunga mazao ya wakulima wakiwa na silaha kali za moto jambo ambalo taarifa zimewasilishwa kwa viongozi bila mafanikio

Maoni