CCM KITETO YAZIDI KUMONG'ONYOKA


CCM Kiteto wazidi kuumbuana

NA MOHAMED HAMAD
HALI ya kisiasa ndani ya chama cha mapinduzi CCM wilayani Kiteto inazidi kuzorota kutokana na wanachama wa chama hicho kuendelea kutuhumiana kwa masuala mbalimbali

Akizungumza hayo Juma Shabani katibu mwenezi wa kata ya bwagamoyo amedai kuwa hayupo tayari kusikia mwanachama akianza katangaza nia yake ndani ya kata hiyo kwakuwa muda wa kampeni bado

Amesema kitendo hicho kitawafanya viongozi waliopo madarakani kushindwa kutimiza wajibu wao badala yake nao wataendeleza kampeni za kuiimarisha kuwa madarakani badala ya kuwatumikia wananchi

Mwanachama huyo wa CCM amemtuhumu katibu mwenezi wa CCM wilaya Christopher Parmeti kuwa ameanza kufanya kampeni ndani ya kata hiyo akisema hakubaliani na kitendo hicho ambacho amedai kuwa kitawagawa wanachama wao

“Siamini mwenezi wa Wilaya Christopher Ole Parmeti anamtendea haki diwani wa kata ya Bwagamoyo Yahaya Masumbuko kwani kama kiongozi alipaswa kusubiri muda wa kampeni badala ya kufanya anachokifanya kwa hivi sasa”alisema Juma

Kwa upande wake Christopher Parmet ambaye pia ni katibu mwenezi CCM wilaya amedai kuwa kinachoenezwa na mwanachama huyo ni uchanga wa siasa  ambao hautakiwi ndani ya chama hicho kwa sasa

Amesema siasa ya leo sio ile iliyofanywa na waasisi kulingana na mazingira yaliyopo akisema ni vyema mwanachama huyo tena kiongozi akaendana na wakati kujua hatua iliyofikiwa kisiasa kwa kupitia vyomba mbalimbali vya habari na hata kuisoma katiba yao

“Natamani ili tuweze kufanana na wanachama wetu kila mtu awajibike kujua majukumu yake ya kisiasa kwani yote haya yanatokana na kujishuhulisha kufuatilia mambo kama vile kusoma magazeti vitabu na hata kusikiliza redio,kuangalia runinga”

Kama tutaendelea kuwa na wanachama kama hawa watatupa taabu sana na ikishindikana tutatazama kanuni na sheria zetu za chama kama kuna haja ya kuea na watu wa namna hii alisisitiza Parmeti huku akisema nawahi kwenye kikao tutaongea

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa hali ya kisiasa si shwari ambapo uongozi wa mkoa umeingia kunusuru huku zikiwa zimebakia siku nne Katibu Mkuu wa CCM Abrahaman Kinana Aug 8  anakusudiwa kufika Manyara kuwasimika makamanda hivyo bado jitihada zinaendelea kunusuru hali hiyo

Mwisho

Maoni