KITETO KUKUMBWA NA NJAA






Hofu ya njaa yaibuka Kiteto


Na. Mohamed Hamad Manyara
Ukosefu wa masoko ya uhakika na kuwepo biashara huria hapa nchini ya mazao  ya nafaka, imeelezwa kuwa unaleta madhara kwa wakulima kuuza mazao yao kwa hasara wakati wote huku Serikali ikiwa kimya


Hayo yameelezwa na wananchi wilayani hapo wakisema hakuna njia mbadala kwani malengo yao ni kukabilina na ugumu wa maisha uliopo maeneo yote hapa nchini yakiwemo vijijini


“Tulitegemea kuiona Serikali ikikabiliana na tatizo hili tena mapema kwakuwa wao ni wasomi na wanajua kusoma nyakati badala yake wako kimya hawasemi nadhani wana lengo lao wanalotaka litimie” alisema Bakari Mainganya (mkulima)


Alisema Serikali imekuwa ya kushugulikia majanga zaidi kuliko kuzuia na ndio maana hakuna mpango unaoonekana kufana katika maeneo yao shuhuli nyingi hazikukamilika kwa madai kuwa Serikali haina fedha


Hali hii imewaacha wananchi njia panda wasijue cha kufanya ambapo alisema wakati wakiingia madarakani walikuwa na mipango madhubuti iliyowafanya waaminike kwa wananchi akihoji  kigugumizi kinatoka wapi cha kuwajibika?


Katika hatua hiyo imeelezwa kuwa gunia moja la mahindi linauzwa kati ya tsh 25,000 na 30,000 wilayani Kiteto huku ikielezwa kuwa kiasi hicho hakilingani na uzalishaji wa mazao hayo kwa mwaka


Naye Hassani Konki {mwananchi) alisema ni vyema Serikali ikawa na utaratibu wa kuwakopesha wakulima fedha wanapokuwa na hitahi hilo huku wakiwa wamehifadhi mazao yao ghalani ili mwiso wa siku wanufaike na kilimo  hicho


“Hapo awali kulikuwa na utaratibu mzuri sana kwa wakulima kwali waliweza kuhifadhi mazao yao na mwisho wa siku waliuza kwa bei ya juu tofauti na ilivyo sasa wakulima wananyonywa hadharani Serikali ikiwa kimya”alisema Konki


Kw siku moja zaidi ya magari aina ya fuso 30 huondoka yakiwa yamejaa mahindi baada ya kununua kwa bei hiyo na kwamba ili kunusuru kuibuka njaa kwa wananchi hao iko haja viongozi hao kuibuka kuokoa jahazi hilo


Mwisho

Maoni