KITETO WAWASHANGAA VIONGOZI WAO KUHUSU MAUAJI

Wananchi Kiteto wawashangaa viongozi wao

-Ni kwa kushindwa kuzuia mauaji ya wakulima,wafugaji

Na.Mohamed Hamad Manyara
Mauaji yanayoendelea kujitokeza kati ya wakulima na wafugaji wilayani
Kiteto yameibua hisia tofauti kwa makundi mbalimbali ya kijamii ambapo
sasa wameamua kuwatuhumu viongozi wao kwa kushindwa kudhibiti vitendo
hivyo

Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema mgogoro huo ni wa muda mrefu
ambao umesababisha viongozi mbalimbali wa Kitaifa kufika akiwemo
Waziri Mkuu Mizengo Pinda,Katibu Mkuu wa CCM Taifa Abrahamani Kinana
na wengine wengi

"zaidi ya wakulima na wafugaji 20 wamepoteza maisha ndani ya miezi
isiyozidi kumi,huku wengine zaidi ya 50 wakiwa wamejeruhiwa vibaya na
kupata vilema vya maisha kutokana na vitendo vya kuvamiana wakiwa
katika shughuli za uzalishaji"

"Hakuna kisichofahamika hapa Kiteto kwa viongozi wetu tulitegemea kwa
mamlaka tuliowapa wangekuwa msaada mkubwa kutatua mgogoro huu badala
yake wamekuwa wabaguzi,wakabila hali iliyofanya tufike hapa"alisema
Maulidi Kijongo {Mkulima}

Alisema kuwa viongozi wa Kiteto hawasemeheki juu ya mauaji
yanayoendelea kujitokeza kila mara kwani wao walipewa mamlaka na
wananchi kusimamia sheria kwa kutumia elimu zao badala yake imekuwa
kinyume chake

Makundi yaliyoonyesha kushangazwa na uongozi huyo ni pamoja na
waangalizi wa haki za binadamu Kiteto,taasisi za kidini, vyama vya
siasa wakisema ukimya wa viongozi hao umechangia kuendelea mauaji

Kwa upande wake Sekemi Sakana (Diwani) wa CCM kata ya Parimbo alisema
mgogoro huo wa ardhi hautatatuliwa na viongozi wa Kiteto kwakuwa
wameshindwa hivyo ameitaka Serikali ngazi ya Taifa kuingilia kati

Alisema tatizo lililopo hakuna kiongozi anayesema ama kusimamia ukweli
juu ya mgogoro huu kwani yanaonekana makundi hayo kugawanywa kwa
itikadi za kisiasa kikabila na hata kwa njia zingine ambazo madhara
yake ni mauaji hayo

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipofika Kiteto kuhusu na mgogoro huo
aliwataka makundi hayo kuridhiana na viongozi wao kuangalia upya
mipango waliyojiwekea ya matumizi bora ya ardhi ili kuzuia mauaji hayo

Agizo hilo limedaiwa kupuuzwa toka mwezi wa pili alipofika hadi mwezi
huu wa nane ambapo toka aondoke mauaji yameendelea kujitokeza kwa
nyakati tofauti kati ya makundi hayo ya wakulima na wafugaji

Kwa Upande wake Abrahamani Kinana katibu wa CCM Taifa alipowasili
Kiteto alisema kuwa alichokiona kinatosha na kwamba ataenda kumweleza
Mhe. Rais ili aweze kuchukuwa hatua dhidi ya viongozi hao ambao
amewabaini

Jumla ya watu watu watano ndani ya siku nne katika maeneo tofauti
Wilayani humo wamepiteza maisha kutokana na kuibuka ghasia hizo ambapo
huwa nyakati za kiangazi na masika

Mwisho

Maoni