MAKALA YA ARDHI
KITETO -1
Migororo ya ardhi
nani alaumiwe Kiteto?
Na.Mohamed Hamad Kiteto.
Kwa mujibu wa vitabu vitakatifu ambavyo vinatumiwa
na makundi mbalimbali ya kijamii vimeeleza kuwa asiyefanya kazi na asile,kauli
hii imewasukuma waliowengi kufanya kazi ili waweze kutafsirika vizuri ndani ya jamii
na nchi yao kwa ujumla.
Msimu wa masika na kiangazi hapa nchini na hasa wilayani
Kiteto mkoani Manyara umekuwa taabu na mateso kwa jamii za wakulima na wafugaji
kwakuwa wamechagua kuendesha maisha yao kwa kufanya shughuli hiyo ama zote kwa
pamoja.
Kutokana na maamuzi hayo kazi hizo zimegekuwa
shubili kwa pande hizo badala ya neema baada ya kuanza kuuana kwa kilichodaiwa
kugombea ardhi kwaajili ya shuhuli za kuliletea maendeleo kilimo na ufugaji
“Baba wa Taifa enzi za uhai wake aliweza kuwakamata
wasiofanya kazi na kuwafungulia mashitaka akiwaita wazururaji hali ambayo wengi
wao walishika adabu na kuanza kufanya kazi ya kujipatia kipato”
“Mimi ni miongoni waliokubwa na sakata hili la kukamatwa
kwa miaka ya nyuma enzi za ujamaa, tulikamatwa na wenzangu kisha kufunguliwa
mashitaka wengi wetu tulikutwa mijini tukitakiwa kurudi vijijini tukalime ama
kufuga”alisema Maulidi kijongo (mkulima)
Hali hii ilitulazimu hata tulipotaka kwenda
kuhitaji bidhaa mijini tuwe makini ili tusikamatwe na kuitwa wazururaji
ikijengwa hoja ya kila mtu lazima afanye kazi ya kumwingizia kipato chake ama
familia yake
Ni kutokana na msingi huo leo utawaona watu
wakilazimika kufanya kazi ingawa ule utaratibu wa kukamatwa tena kwa madai ya
uzurura mijini haupo lakini kuna changamoto kibao zinazotokana na kufanya kazi
Mkulima huyo alitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa
ni pamoja na uzalishaji wa mazao hayo kwa shida aidha iwe ya mifugo ama kilimo
kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo
za kusababishiwa ama za kimazingira
Akizungumza bila kumumunya maneno mkulima huyo
ataja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni migogoro ya ardhi ambayo imekuwa tishio
kwa maisha ya wananchi ambayo imedaiwa kusababishwa na baadhi ya viongozi wasio
kuwa waadilifu
Migogoro hiyo imeelezwa kuwa imetokana na makundi
hayo ndani ya jamii kugombanishwa kwa maksudi na baadhi ya watawala wasio kuwa
waadilifu wakinufaika na ugomvi huo ambao mwisho wa siku watu wanapoteza maisha
Uchunguzi uliofanywa na makala hii umebaini kuwa
kuna baadhi ya viongozi wa ngazi za vitongoji,vijiji, kata,na hata Wilaya
wamekuwa na mamlaka ya kuuza ardhi kwa wanaohitaji huku wakijua eneo hilo sio mahsusi kwa kazi husika
Pamoja na kubainika kwa watawala hao hakuna hatua
iliyowahi kuchukuliwa dhidi ya viongozi hao na watawala wa ngazi ya Wilaya na
hata mkoa jambo ambalo limedaiwa kuzoeleka na hakuna wa kumdhibiti mwnzake
Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Jaki Umbulla ni
miongoni mwa viongozi walioweza kuzungumza hadharani kuwa kuna baadhi ya
viongozi wasio waadilifu tena akiwa na taarifa za uhakika kuhusu viongozi hao
“Kuna baadhi ya viongozi wenzetu wasio waadilifu
ndani ya jamii wamekuwa tatizo kubwa
katika migogoro ya ardhi na hili nawataka wajirekebishe mara moja kwani madhara
makubwa yanazidi kujitokeza”alisema Umbulla
Wakati mwingine unakuta mtu anauziwa ardhi na
kiongozi kufanya kazi ya kilimo wakati eneo hilo ni la mifugo ama kufanya kazi
ya mifugo wakati eneo hilo ni kilimo hali hiyo imefahamika na hakuna hatua
zinazochukuliwa”alisema Bakari maunganya (mkulima)
Alisema malalamiko hayo yamewasilishwa kila kona ya
wilaya mkoa na hata Taifa cha ajabu hakuna hatua iliyowahi kuchukuliwa ya kuwaadhibu
viongozi na hata wananchi waliohusika kukiuka sheria hizo
“Wakati mwingine mtu unasema labda nimekuwa kero
ndani ya Ofisi za Serikali kwani kila mara lazima kuripoti kueleza matatizo
yetu, chaajabu hatuoni hatua zozote ni kulindana tu kwa Serikali hii inaumiza
sana”alisema kwa hisia kali
Kila mara wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto
wamekuwa wakipoteza maisha ambapo mapema mwaka huu mwezi wa pili mwaka huu zaidi
ya watu kumi waliuawa kinyama huku kila baada ya muda wengine kadha nao
hupoteza maisha na hivi karibuni Aug 7 zaidi ya watu watano waliuawa
ITAENDELEA WIKI IJAYO…..
Maoni
Chapisha Maoni