Mabadiliko
tabia ya nchi yaathiri wananchi Kiteto
Na.Mohamed hamad Manyara
MABADILIKO ya tabia ya nchi
yanayotokana na sababu mbalimbali nchini zikiwemo uharibifu wa mazingira
yameanza kuleta madhara kwa wananchi wilayani kiteto mkoani Manyara yakiwemo uhaba
wa maji, pamoja na kuibuka kwa magonjwa ya binadamu na mifugo
Wakizungumza kwenye mafunzo
ya siku moja wadau wa mabadilko ya tabia ya nchi yaliyoandaliwa na shirika la Msalaba
Mwekundu Kiteto walisema madhara makubwa yanayoendelea kujitokeza na kuwataka wananchi
kuwa tayari kukabiliana na janga hilo
Mratibu wa shirika la
msalaba mwekundu wilayani Kiteto Miraji Salmu alisema madhara yanazidi kujitokeza kutokeza
kutokana na kukosekana taarifa sahihi za hali ya hewa pamoja na elimu duni ya
namna ya kufikia taarifa hizo
“Madhara ya mabadiliko ya
tabia ya nchi yanazidi kujitokeza ambapo Kiteto ni moja kati ya wilaya mbili
Tanzania zilizoteuliwa kukabiliana na janga hili ambapo kwa Afrika nchi ya Tanzania
na Malawi ndio zilizopendekezwa kukabiliana na janga hilo”alisema Miraji
Akieleza mipango na mikakati
ya kukabiliana na janga hilo mkurugenzi mtendaji wa shirika la msalaba mwekundu
Tanzania Renatus Mkaruka alisema shirika lake limeamua kuunganisha nguvu ya
pamoja na mashirika mengine ulimwenguni kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya
nchi
Alisema watafanya kazi kwa
kushirikiana na mashirika mengine katika kukabiliana na janga hilo yakiwemo
shirika la Afya Duniani (WHO),mamlaka ya
hali ya hewa Tanzania (TMA), shirika la chakula duniani (WFP) na UDSM ambayo
kwa pamoja yatafanya kazi tofauti
Bw.Mkaruka ametaja maeneo
yatakayo shughulikiwa kuwa ni pamoja na umoja na kuangalia usalama wa chakula, lishe, afya,
pamoja na namna ya kupunguza athari za maafa ndani ya jamii
Akieleza historia ya mradi
huo Mecklina Merchades kutoka mamlaka ya hewa Tanzania (TMA) alisema mchakato
wa kukabiliana na janga hilo ulianza mwaka 2009 huko Geniva ya uswisi ambapo
nchi kadhaa zilikutana kujadili namna ya kukabiliana na janga hilo
“Watafiti wamegundua kuwa
majanga yataendelea kujitokeza hivyo mradi huu utasaidia kuwapa elimu wananchi
ya jinsi ya kukabiliana na majanga hayo ambayo madhara yake ni kupoteza maisha
ya viumbe hai wakiwemo wanadamu na hata mifugo”alisema
Alitaja baadhi ya maengo ya
mradi huo kuwa ni pamoja na kupunguza athari zinazotokana na mabadiliko ya
tabia ya nchi, kufanikisha kutekelezwa kwa malengo ya nchi, taarifa kutumika
katika mipango ya utekelezaji,pamoja na kuboresha miundombinu iliyopo
Kwa upande wake Amani
Abrahamu (mfugaji) alisema madhara yanayoendelea kujitokeza katika maeneo ya
Makami wilayani Kiteto ni pamoja magongwa ya mifugo kuendelea kuibuka, na ya
binadamu hali inayotishia kizazi cha jamii ya kifugaji kutoweka
“Sisi wafugaji wa jamii ya
kimasai hatuna utamaduni wa kuweka fedha benki na ndio maana tunawekeza kwenye
mifugo tukielezwa kupunguza mifugo kutokana na janga hili ni sahihi ila elimu
zaidi inatakiwa kutolewa kwani hakuna mfugaji anayeridhia kwa hivi sasa
Zaidi ya washiriki 20 kutoka
mashirika ya umma yanayofanya kazi zinazofanana katika kukabiliana na tabia ya
nchi likiwemo shirika la KINNAPA,NAADUTARO,na watendaji wa vijiji vinavyotekeleza
mradi huo vya Orpopong’i, Ndaleta, makami, na Ndedo wameshiriki katika warsha
hiyo ya siku moja mjini Kibaya
Mwisho
Maoni
Chapisha Maoni