Migogoro
ya ardhi Kiteto ikomeshwe-4
Na.Mohamed Hamad Kiteto
MAKALA
iliyopita iliishia sehemu inayosema kuwa, kama Rais atakuwa ameamua kumtuma kwa
mara nyingine Waziri Pinda basi aje
kuonana na wananchi wenyewe ambao ni wakulima na wafugaji kila mmoja aseme nani
alihusika na kwa kiwango gani kuchangia mgogoro huo na sio kuongea na
waliosababisha wa mgogoro peke yao.
Wiki hii makala inaangazia
hatua ya mgogoro wa ardhi Kiteto mkoani Manyara kutinga Bungeni kutaka msaada
zaidi ili kunusuru maisha ya wakulima na wafugaji wanaoendelea kuhasimiana kila
kukicha yalindwe baada ya kuonekana kuwa hatarini
Wakati mwingine wakulima na
wafugaji wilayani Kiteto wamedai kuwa wanaisha maisha ya wasiwasi wanapofanya
shughuli zao za kujitaftia riziki kutokana na uhasama uliojengeka kati yao
Malalamiko hayo
yamewasilishwa kwa viongozi mbalimbali wa chama na Serikali katika ngazi
tofauti hapa nchini kunusuri, lakini bado hali inazidi kuwa tishio na wakati
mwingine wananchi hao wamedai kuwa sasa wameamua kumwachia Mungu
Wakati kauli hiyo ikionekana
kuwa ni ya kukata tamaa dhidi ya viongozi wao ambao wamedai wameshindwa
kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo unaosababisha mauaji ya mara kwa mara mgogoro
huu umetinga Bungeni
Katika kuwahakikishia
Watanzania kuwa suala hili Serikali imeamua kulivalia njuga Mbunge wa viti
maalumu mkoa wa Manyara na Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha Jaki Umbula
aliibukia Bungeni na kusema Waziri Pinda ameshakabidhiwa kazi hiyo
Alisema suala hili linashuhulikiwa
kwa undani kwani baada ya tatizo hili kuonekana kwa viongozi wa ngazi za juu
akiwmo Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika ziara yake ya mkoa wa Dodoma alisema
suala hili litashuhulikiwa na Waziri Mkuu Pinda
Alisema pamoja na mambo
mengine alichojifunza akiwa Bunge la Katiba ni pamoja na maridhiano kwa viongozi wanapowaongoza
wananchi na pasiwepo na tabia za kujitaftia umaarufu majukwaani
Akichangia taarifa kamati za
Bungeni la katiba Martha Jaki Umbulla alisema “mgogoro wa ardhi unahitaji
maridhiano ya viongozi na si kwenda majukwaani inachochea uhasamakati ya
viongozi na hata wananchi wenyewe”
“Nimejifunza kitu kizuri
sana, maridhiano ni nmuhimu badala ya viongozi kwenda kwenye majukwaa ya
kisiasa na kuzungumzia migogoro na kuzidi kupanua wigo wa mitafaruku ni vizuri
tukarudi kwenye maridhiano”
“Sitaki kuingia kwa undani
sana kwasababu Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania analishuhulikia
kwa ukaribu na hata Rais wetu akiwa katika ziara yake Dodoma aliliona na kusema
litashuhulikia kwa umakini zaidi”alisema Umbula
Hata hivyo kauli hiyo
imetokana na lalamikola la Mbunge wa Kongwa Job Ndugai kuwa Rais Jakaya Kikwete
akiwa ziarani Kongwa alilalamikiwa juu ya mauaji yanayoendelea kujitokeza kila
mara wilayani hapo
“Mheshimiwa Rais, kule
Kiteto ni majirani zetu kuna mauaji ya kutisha kila mara napokea maiti za watu
wangu waliouawa huko mashambani kuna uongozi lakini uko kimya na hawajawahi
hata siku moja kushiriki mazishi hali hii inasononesha sana naomba kauli ya
Serikali”alisema Ndugai
Wakulima kutoka maeneo ya
Kongwa wanauawa na kuambiwa kuwa ni wavamizi Serikali ina mpango gani
kuwasaidia watanzania hawa wasio na hatia?huu ubaguzi ni mpaka lini mbona Baba
wa Taifa alikemea”alisema Ndugai huku akionyesha kukerwa na kitendo hicho cha
mauaji
Hata hivyo kuwasilishwa kwa taarifa
hiyo Bungeni na Mb. Viti maalumu mkoa wa Manyara Martha Umbulla kumetafsiriwa
kuwa ni kujibu shambulizi dhidi ya Mbunge wa Kongwa Job Ndugai na Chemba Juma
Nkamia kuhusu kuendelea kuutuhumu uongozi wa Kiteto kushindwa kuzuia mauaji ya
watu wasiokuwa na hatia
Waharakati wa haki za
Binadamu wameelezea hali inayoendelea kujitokeza Kiteto ni kukwepa majukumu kwa viongozi hao na kwenda
kuongelea suala hili Bungeni kwani awali walipaswa kudhibiti mauaji kabla ya
kujitokeza
Mashaka Saidi Fundi mwangalizi
wa haki za binadamu Wilayani humo alisema mgogoro wa ardhi Kiteto umedumu kwa miaka
mingi huku kukiwa hakuna dhamira ya dhati kutatua huku sheria zikiendelea
kukiukwa na viongozi
Alisema chanzo cha mgogoro
huo ni mkanganyiko wa kuanzishwa hifadhi ya jamii ya Emboley Murtangos ambayo
ilidaiwa kuwa chini ya vijiji saba vilivyoizunguka kuwa hakukuwa na dhana
shirikishi bali kulikuwa na ujanjaujanja
“Hakuna Kiongozi mkweli
anayezungumzia mchakato wa kuanzisha hifadhi hiyo kuwa itamnufaisha nani kwani
hata baadhi ya vijiji vilivyodaiwa
kutenga eneo hilo vinalalamika kuwa hawakushiriki kikamilifu”alisema Fundi
Alisema malalamiko haya yanatia
shaka kubwa kisheria ambapo kwa hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Martha
Jaki Umbula akiongea na vyombo vya habari alisema hata mihutasari yenyewe ya vijiji vilivyounda
hifadhi ya Emboley Murtangos baadhi ilibwa
Akiongea kwa kujiamini Fundi
alisema suala hili ana nia ya kuifikisha Halmashauri mahakamani kwa kutumia
mamilioni ya fedha kwaajili ya zoezi hilo ambalo hata watunga sera wenywe
madiwani wamekuwa wakitofautiana katika
kulishuhulikia
“Nitakwenda mahakamani
kuishitaki Halmashauri kwa kujiingiza kwenye mgogoro wa vijiji ambao hauko
rasmi kwani inaonekana suala hilo kama linashuhulikiwa kimila na kiukabila
zaidi”alisema Fundi na kuongeza
Tulishuhudia wafufaji
wakilalamika mbele ya Waziri Mkuu Pinda kuchangishwa mamilioni ya fedha
kwaajili ya kuendesha kesi dhidi ya wakulima jambo hili lina utata mkubwa
linahitaji ufumbuzi wa kisheria”alisisitiza
Alisema hata kama mihtasari imeibwa
Serikali ya Kiteto itahakikisha kuwa inapatikana kwani nia na dhamira ya
kuanzishwa hifadhi ipo na watu wapo hivyo hauwezi kukwamishwa na watu wachache
wasio kuwa na nia njema alisema Umbulla
Pamoja na suala hili kutinga
bungeni na kuzungumzwa kama tatizo bado Waziri Mkuu ametwishwa zigo hili
kutafuta ufumbuzi watu wasiendelee kuuana na nnjia pekee ya kutumia ni
kutafutwa uhalali ya kuanzishwa hifadhi hiyo na manufaa yake
masarade1995@gmail.com 0787 055 080
Maoni
Chapisha Maoni