Waziri Mkuu Pinda akiwa ziarani Kiteto kuhusu migogoro ya ardhi
Migororo
ya ardhi Kiteto nani alaumiwe?
Na.Mohamed Hamad Kiteto.
MAKALA ya wiki iliyopita
iliishia sehemu inayosema kuwa Kila mara
wakulima na wafugaji Wilayani Kiteto wamekuwa wakipoteza maisha ambapo mapema
mwaka huu mwezi wa pili zaidi ya watu
kumi waliuawa huku kila baada ya muda
wengine kadhaa hupoteza maisha…
Kutokana na mgogoro huu
makundi mabalimbali ya kijamii wasomi na hata watu wa kawaida kabisa wameweza
kuzungumzia sakata hili ambapo makala hii imeamua kuwapa nafasi ili uweze kujua
mgogoro wa ardhi Kiteto nani alaumiwe?
Awali miaka ya 1992 Shirika
la (LAMP) Land Manegement Programme lililokuwa chini ya SIDA kutoka Sweden liliwezesha
zaidi ya vijiji 35 wilayani kiteto kupanga matumizi bora ya adhi ili kuondoa mgogoro
wa wakulima na wafugaji
Kwa mujibu wa Viongozi wa
shirika hilo na pia uongozi wa Wilaya ya Kiteto walikiri kutumia mamilion ya
fedha katika mipango hiyo ili kuondoa mgogoro kati ya makundi hayo
Kadiri siki zilivyozidi
kuongezeka watu na mifugo iliongezeka na migogoro iilijitokeza huku kukiwa na
mamlaka za ukabiliana na tatizo hilo na wasiweze kuzua migogoro hadi hatua ya
mauaji ilipoweza kujitokeza
Kwa mujibu wa kauli za
viongozi Wilayani Kiteto wamekuwa wakisema chanzo cha migogoro hiyo ni watu kutoka nje ya Wilaya ya Kiteto kuvamia
maeneo kwa kufanya shughuli za kilimo
Mainge Lemalali Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto alikaririwa katika moja ya vikao vya
Halmashauri akisema watu wa Wilaya ya
Kongwa wamekuwa tatizo Kiteto kuvamia maeneo yao na kufanya shuhuli za kilimo
“Kwa sasa hatuhitaji kuona
Kiteto inageuka kuwa jangwa kama ilivyo maeneo mengine na hapa nchini
nasisitiza kuwa yoyote atakaye ingia bila taarifa na kufanya shuhuli za kilimo
huko maeneo tuliyokataza sheria itafuata mkondo wake”alisema Lemalali
Mbali na kauli hiyo pia
Lemalali alitoa wito kwa Serikali ngazi ya Taifa kuingilia kati mgogoro huu
ambao hata wao wamedai umewashinda kwani waliopo katika maeneo hayo ni baadhi
ya vigogo ambao wamejichimbia mizizi katika mapori yaliyohifadhiwa ya Emboley
Murtangos
“Tumetumia gharama kubwa
sana kuwaondoa wakulima waliopo katika maeneo tuliyotenga na hapa naweza kusema
kuwa ni zaidi ya mamilioni ya fedha yaliyotumika lakini bado watu hawatoki na
wanaendelea na uharibu mazingira uongozi
wa juu uingilie kati”alisema Lemalali
Mbali na kauli hiyo pia
alimtaka Mbunge wa Kongwa ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Jobu Ndugai kuwakataza wananchi wake ambao wamevamia
maeneo ya kiteto na wameapa kutotoka kwa madai wako kihalali
“Nimtake tu Kiongozi wetu
Ndugai atumie fursa aliyonayo kuongea na wananchi wake wasivamie maeneo ya
Kiteto na kufanya shuhuli za kilimo ambazo zimekuwa na madhara kuharibu
mazingira Kiteto hatutaki kuharibiwa maeneo yetu na wavamizi”alisisitiza Mainge
Kwa upande wake Job Ndugai
akiongea kwa njia ya simu juu ya wananchi wake kudaiwa kuvamia eneo la kiteto na
kufanya uharibifu wa mazingira alisema anasikitishwa na kauli za kibaguzi
zinazotolewa na viongozi wa Kiteto kuwaita Watanzania wenzao kuwa ni wavamizi
Sidhani kama tumefikia hatua
ya kuitana wavamizi ndani ya nchi yetu, Baba wa Tifa Mwalimu Julius Nyerere
alikemea sana vitendo vya ubaguzi kwa itikadi za kidini kikabila na hata rangi
na kwamba amewataka wananchi wawapime viongozi hao
“Wananchi muwapime viongozi
wenye sura za ubaguzi na niwaombe kila Mtanzania ana haki ya kuishi mahali
popote ilimradi asivunje sheria sasa kama kuna aliyevunja sheria tena kwa
kufanya kazi sio kuiba ama kufanya uhaini
hapaswi kuuawa bali sheria ifuate
mkondo wake
Alisema kila mara mauaji
yamezidi kujitokeza Kiteto na wanaouawa ni watanzania wa Wilaya ya Kongwa mkoani
Dodoma jirani na wilaya Kiteto hivi nani anayewaua Watanzania hawa na huko
Kiteto hakuna viongozi wa kushuhulikia matatizo haya
Naiomba Serikali ngazi ya
juu iweze kuingilia kati kuokoa watu hawa ambao wanauawa bila hatia na kikundi
cha watu wachache wanaojiita walinda mazingira na ambao hawajakamatwa mpaka
leo… alisema ndugai kisha simu yake kukatika
Kutokana na mgogoro huu
viongozi mbalimbali wa ngazi ya Mkoa na Taifa wa chama na Serikali walifika
Kiteto kushuhudia mauaji hayo na pia wengine walifika kutaka kujua kilichopo
hali iliyotafsiriwa kuwa kazi hiyo bado ni ngumu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda ni
miongoni mwa viongozi wakuu ngazi ya juu Serikalini aliofika Kiteto na kuahidi
kuwa suala hili ataenda kuongea na Mhe Rais Kikwete toka mwezi wa pili mwaka
huu
Na hata hivyo baada ya
kuondoka mauaji yaliendelea ambapo zaidi ya watu nane waliuawa kikatili
kukatwakatwa mapanga na wengine kuchinjwa wakigombea ardhi
Hali kadhalika Katibu Mkuu
wa chama cha mapinduzi CCM Abrahamani Kinana alifika Wilayani humo kuongea na
wananchi ambapo alisema kuna matatizo lukuki na ambayo kwa nafasi yake
atahakikisha kuwa anakaa na Rais Kikwete kumweleza alichokiona
Hata hivyo Rais Kikwete
katika ziara yake mkoani Dodoma alilalamikiwa na wananchi kuwa kila mara
wameendelea kupokea maiti za ndugu zao wanaouawa katika maeneo ya kiteto hivyo
wamechoka na kumtaka Rais atoe tamko
MAKALA ITAENDELEA WIKI
IJAYO…
Maoni
Chapisha Maoni